Na John Walter-Manyara
Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), umefadhili Minara ya makampuni ya mitandao ya simu 54 katika kata 42 Mkoani Manyara.
Hayo
yamesemwa na Mhandisi Mwandamizi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote,
Baraka Elieza, wakatika akizungumza na Waandishi wa habari Mkoani hapa
katika ziara ya Naibu waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya
habari amesema kuwa Minara yote walioifadhili imekamilika isipokuwa
Minara miwili ambayo itakamilika mapema mwaka huu.
Ameitaja Minara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni ni katika Kijiji cha Sigino pamoja na Kijiji cha Himiti.
Akizungumzia
mipango ya mfuko huo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), kwa mwaka wa
fedha 2021_2022, nikutekeleza ujenzi wa Minara katika kata 15 ndani ya
mkoa wa Manyara.
Amesema wamejikita katika maeneo ya vijijini na
baadhi ya maeneo ya mijini, ambapo Kuna usikivu hafifu wa mawasiliano,
kwa kutoa ruzuku kwenye makampuni ya mitandao ya simu ili wapeleke
huduma ya mawasiliano kwa wananchi, pamoja nakupeleka mawasiliano ya
redioni katika maeneo ambao Kuna usikivu hafifu wa redio.
Aidha mfuko
huo unafundisha walimu Mafunzo ya tehama, ili waweze kupata ujuzi,
pamoja nakupeleka kompyuta katika shule za serikali, ikiwa lengo
nikuunganishe shule hizo na intaneti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...