NA MWANDISHI WETU

MBUNIFU nguli wa mavazi hapa nchin Martin Kadinda, anatarajiwa kutambulisha collection yake Mpya mavazi Aliyoipa Jina la Escapade  katika onyesho la ubunifu wa mavazi lenye dhima ya kuhamasisha utalii  mkoani Manyara katika hoteli ya Mawe mawe Januari 29.

Hii itakuwa ni onyesho lake la kwanza kwa mwaka huu kushiriki hapa nchin mara ya mwisho alitambusha collection ya Vanguard, katika tamasha la Swahaili Fashion Week 2020.

Akizungumza na ukurasa huu amesema dhumuni la Escapade collection ni kushawishi watanzania kufanya utalii wa ndani wakienda mbugani katika mavazi yanayo kwenda na wakati.

"Tanzania tuna vivutio vingi ndani ya miaka miaka miwili tumepata muamko mzuri wa kutembelea vivutio vyetu ila wengi wamekuwa wakipata shida katika upande wa mavazi ndio maana nimebuni Escapade collection ambayo ni mwendelezo wa collection yangu ya mwaka 2020 Vanguard , kwa ajili ya kuleta umaridadi wakati wa safari za utalii wa ndani," anasema Martin Kadinda.

Aliongeza kuwa kabla ya onyesho hilo kesho atashiriki kuuza vifaa mbalimbali alivyo tengeneza  vinavyotumika katika safari za utalii katika mnada utakaofanyika katika hoteli ya Mawe mawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...