Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amemtaka mkandarasi wa mradi
wa maji wa Kigamboni mpaka inafika mwezi Aprili mwaka 2022 kuwa
ameishamaliza ujenzi wa mradi huo.
Ameyasema
hayo alipotembelea mradi wa maji wa Kigamboni unaojumuhisha ujenzi wa
tenki kubwa la kuhifadhia maji litakolokuwa na ujazo Lita Milioni 15
pamoja na uchimbaji wa visima katika eneo la Kigamboni.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara hiyo amesema
anamtaka mkandarasi wa mradi huo kuendana na muda waliojiwekea na kama
akishindwa kuendana makubaliano ya mradi basi watavunja mkataba kwani
anawachelewesha wananchi wa Kigamboni kupata maji safi.
"Rais
Samia anasisitiza wananchi kupata maji safi na salama lakini inaonekana
mkandarasi huyu anataka kukwamisha juhudi zake hivyo hatutaivumilia
kasi anayokwenda nayo mkandarasi wa mradi". Alisema Luhemeja.
Pia Mhandisi
Luhemeja amempongeza Mkandarasi anayetoa maji visimani kwa kukamilisha
ununuzi wa pampu tatu za kusukuma maji, huku akimuagiza kuongeza kasi
katika mchakato wa manunuzi ya pampu za kutoa maji visimani kupeleka
kwenye tenki.
"Namuagiza
Mkandarasi kukamilisha manunuzi hayo mapema ifikapo mwezi wa pili Ili
kukamilisha mradi huu, endapo ifikapo mwezi wa nne Mkandarasi hajamaliza
mradi tutamwondoa," amesisitiza Mhandisi Luhemeja.
Amesema
shughuli
ya usambazaji wa mabomba kupitia mradi huu wa maji Kigamboni
unatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 17/1/2022 hivyo ametoa maagizo kwa
Menejimenti ya DAWASA kuhakikisha wanaendeleza mapambano
kukamilisha mradi huu ndani ya Muda.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akikagua Pampu za kusukumia
maji zitakazotumika kwenye mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa ziara ya
kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Miradi na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi.
Mkurugenzi
wa Miradi na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi(kulia) akitoa
maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu visima
vilivyojengwa pamoja na maeneo yatakayojengwa Pampu za kusukumia maji
kwenye mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya
Maendeleo inatekezwa na DAWASA
Baadhi ya Pampu za kusukumia maji zitakazotumika kwenye mradi wa maji wa Kigamboni
Mhandisi
Mshauri wa Mradi wa Maji Kigamboni, Beda Lyimo akitoa maelezo kwa Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu wanavyoendelea na
ujenzi wa Kituo cha kusukumia maji cha Kimbiji wakati wa ziara yake ya
kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akikagua Tanki litakolokuwa na
ujazo wa Lita Milioni 15 kwenye mradi wa maji wa Kigamboni wakati wa
ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kumaliza kutembelea mradi wa maji wa Kigamboni
wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inatekezwa na DAWASA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...