Msemaji Mpya na Mkuu wa Kitengo cha Habari,
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi leo tarehe 24 Januari 2022 amefanya ziara
ya kujitambulisha na kuongeza uhusiano baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na
Jeshi la Uhamiaji nchini katika Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma.
SACF Nzalayaimisi alipokelewa
na Msemaji wa Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle na baadae kukutana na Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala kwa ajili ya kujitambulisha.
Dkt. Makakala amempongeza SACF Nzalayaimisi kwa
kuteuliwa nafasi ya kuwa Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kumtakia
mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya Taifa.
Aidha Kamishna Jenerali Dkt. Makakala amevitaka
vitengo vya Habari Mawasiliano na Uhusiano katika majeshi hayo kuendeleza
uhusiano na ushirikiano ili kubadilishana uzoefu katika kazi mbalimbali za
kihabari.
Kwa upande wake Msemaji Mpya wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji SACF Puyo Nzalayaimisi, amelishukuru Jeshi la Uhamiaji kwa
kuimarisha uhusiano uliopo wa kutekeleza majukumu ya habari na elimu kwa umma
kupitia mitandao ya kijamii na kuahidi kwamba wataendelea kujifunza namna Jeshi
la Uhamiaji linavyotekeleza majukumu yake ya kuhabarisha umma kupitia mitandao
ya kijamii na njia nyingine mbalimbali za kidijitali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...