Aliyekuwa Mtangazaji wa Azam TV Ahmed Ally leo Jumatatu Januari 3,2022 ameteuliwa kuwa Afisa Habari na Mawasiliano katika Klabu ya Simba SC.
Kabla ya kutangazwa kuwa Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alikuwa mtangazaji wa Azam TV, lakini kabla ya hapo aliwahi kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye kampuni ya Sahara Media (Radio Free Africa na Star TV).
Kupitia ukurasa wa Facebook wa Simba SC wameandika:
"Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.
Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano. #NguvuMoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...