TAASISI ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu (Peace Life for Person with Disability Foundation (PLPDF)), imepokea msaada wa vifaa visaidizi wakati wa ujenzi wa vyoo rafiki kwa wanafunzi wenye mashuleni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Januari 28, 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Sophia Mbeyela Maarufu kama Madam Sophy amewashukuru Goodeletronics hardwere wa kutoa vifaa hivyo.
Amesema kuwa kwa kuanzia matundu 20 ya vyoo vya mfano yatajengwa katika shule tano za jijini Dar es Salaam ambazo ni Shule ya sekondari Jangwani na Pugu, pamoja na shule za Msingi ambazo ni Maarifa, Viwegeni na Yangeyange zilizopo Chanika.
Sophia amesema kutokana na utafiti walioufanya wameona kuna wanafunzi walemavu wengi ndio sababu iliyochangia kujenga vyoo hivyo katika shule hizo.
"Mapokeo makubwa ya wazazi kuwapeleka watoto shule na hamasa kutoka kwa Serikali juu ya kila mtoto kuhakikisha anaenda shule bila kujali hali yake ndio hasa sababu ya kujenga vyoo rafiki." Amesema Sophia
Amesema idadi ya matundu ya vyoo yaliyopo ya sasa ni vichache kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni.
Amesema kuwa kampeni iliyozunduliwa Julai 14, 2021 imesaidia kupata kiasi cha shilingi milioni 10 kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa vyoo rafiki kwa wanafunzi walemavu waliopo shuleni pia kunamdau ambaye hakutaka jina lake kutajwa kwa kuchangia masinki ya vyoo 24 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo vya mfano mashuleni.
Amesema kuwa Kwa choo chenye chumba kimoja kinagharimu shilingi Milioni tatu na laki tano na sabini (3,570,000/#) na kwa shule zote tano inahitajika shilingi milioni 89,250,000/#.
Amesema ujenzi wa vyoo rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu vyenye matundu matano kwa shule moja unagharimu kiasi cha shilingi milioni 17, 850,0000/#.
Hivyo amewashukuru wadau waliotoa mchango wao pia ujenzi utaanza hivi karibuni baada ya kukaa kikao na mkurugenzi.
"Niwaombe wadau, kampuni muendelee kuchangia ili kuweza kufanikisha jambo hili kwa jamii kwa sababu ni manufaa kwetu sote." Ameomba Sophia
Ameomba wadau wanaoweza kuchangia wachangie kwa LIPA namba ya M-PESA 5555777 na namba ya Akaunti ya Benki ya NMB 22510027964 kwa jina la PLPDFF.
Hata hivyo ameomba serikali inapojenga shule mpya isiwasahau watu wenye ulemavu kuhusu miundombinu yao pamoja na vyoo rafiki.
Kwa Upande wake GoodCharles stone, Meneja wa duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Good eletronics hardwere, amewaomba wadau wengine wanaoweza kuchangia wachangine ili watoto walemavu wapate haki sawa na watoto wa kawaida.
Amesema wanafunzi wenye ulemavu wamesahaulika sana wameona wamuunge mkono Sophia kwa kuchangia vifaa vya shilingi laki tano.
"Niwahamasishe wauza hardwere wengine waliopo kariakoo waweze kuchangia kampeni ya Sophia kwa kujenga vyoo Rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu mashuleni."
Amesema kuwa kwa watu wachache kampeni hiyo haiwezi kufanikiwa lakini kwakuungana itafanikiwa kwa wakati na kufikia lengo lililokusudiwa.
Meneja wa duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Good eletronics hardwere GoodCharles stone akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022 kushoto ni Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu (Peace Life for Person with Disability Foundation (PLPDF)), Sophia Mbeyela.
Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu (Peace Life for Person with Disability Foundation (PLPDF)), Sophia Mbeyela Maarufu kama Madam Sophy kulia akizungumza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Januari 28, 2022 mara baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu (Peace Life for Person with Disability Foundation (PLPDF)), Sophia Mbeyela akipokea msaada kutoka kwa GoodCharles stone, Meneja wa duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Good eletronics hardwere jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...