Halmashauri ya Chalinze imekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa fedha za Uviko.
"Tarehe 4 Januari 2022, ilikuwa siku nzuri sana kwa wananchi wa Chalinze baada ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kupokea vyumba vya madarasa 80 yakiwemo Madarasa ya sekondari 66 na Shule ya Msingi shikizi 14 kwa upande wa Elimu,"
" Milioni 80 kwa ajili ya Bweni la wanafunzi wenye uhitaji maalum shule ya msingi Chalinze, Milioni 90 Nyumba ya Mganga Tatu kwa Moja Hospitali ya Wilaya Chalinze inayojengwa Msoga kutoka kwenye Fedha za Uviko.alisema mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.
Ridhiwani alieleza, kazi inaendelea ya kujenga maendeleo ya Watu.
Shukrani za Wana Chalinze kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali maisha ya Watanzania anaowaongoza. "Kazi yetu ni kuhakikisha Ndoto na Maono yake yanatimia.
#KaziInaendelea #SSH #MamaKazini #TukoPamojaNaMama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...