WAZIRI wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk.Dorothy Gwajima amesema Serikali itahakikisha kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Taifa kuna mifumo madhubuti ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa dawati la kijinsia na mradi wa Our Right,Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) ambapo amefafanua wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Kati wamekuwa wahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyowasababishia uzorotaji wa masomo yao.

Waziri Dk Gwajima amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo Serikali kupitia Wizara anayoisimamia wameandaa mpango mkakati wa kuanzisha dawati la kijinsia ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoghalimu maisha ya wanafunzi.

Ameongeza kwamba kuna  matukio mengi ya ukatili wa kijinsia  yanaongezeka siku hadi, hivyo wakati umefika sasa wa kutokomeza haya yote kwa kuwepo kwa dawati la kininsia kila chuo na kusisitiza madawati hayo yanatakiwa kuwa madhubuti na yanayofanya kazi kwa vitendo.

Dk Gwajima amesema watakuwa wanafanya ziara ya mara kwa mara kutembelea madawati hayo ili kuona ufanyaji wake wa kazi unavyotendeka." Serikali haijawahi kukaa kimya kuhusiana na ukatili unaoendelea katika vyuo tayari ilishaanzisha vituo mbalimbali vya kisheria".

Awali Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga amesema  mradi wa 03 utanufaisha vyuo vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).Pia mradi huo utaleta manufaa katika vyuo vikuu na vya kati katika kupambana na vita dhidi ya ukatili wa kikinsia.

Kipanga amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kikamilifu kuondoa changamoto ya ukatili wa kijinsia. 

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Profesa,William Anangisye ameeleza  mradi wa 03 una malengo matatu ya kuondoa utotoni,kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia katika vyuo vikuu.

Akizungumza mbele ya Waziri na viongozi wengine wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mwakilishi wa UNESCO nchini Tirso Santos amesema lengo la kuleta mradi huo ni kutaka kuona wanafunzo wa vyuo vya juu wanasoma huku wakijiamini.

Amesema anatambua kumekuwepo na changamoto ya kijinsia inayowakumbwa wanafunzi wa kike na hivyo umesababisha baadhi yao wawe wanasoma bila ya kujiamini kwa sababu ya kupata changamoto za ukatili wa kijinsia,hivyo ni matarajio yao mradi huo unakwenda kuondoa hali hiyo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk.Dorothy Gwajima akizindua dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mradi wa Our Right,Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) leo jijini Dar es Salaam, Kushoto kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Juma Kipanga sambamba na Wadau wengine mbalimbali kutoka meza kuu wakishuhudia uzinduzi huo.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR -MMG.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk.Dorothy Gwajima akizungumza mbele ya Wageni na Wadau waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na mradi wa Our Right,Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) leo jijini Dar es Salaam

Waziri ni Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Juma Kipanga akifafanua jambo mbele ya Wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya  uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na mradi wa Our Right,Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) leo jijini Dar es Salaam


MKurugenzi na Muwakilishi wa UNESCO kwa Kanda ya Afrika Mashariki Prof.Hubert Gijzen akizungumza mbele ya Mgeni rasmi na Wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya  uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na mradi wa Our Right,Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) leo jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Uswisi,Leo Nascher akizungumza mbele ya Mgeni rasmi na Wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya  uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na mradi wa Our Right,Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO ) leo jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Meza kuu ikishuhudia yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo kabla ya uzinduzi









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...