Viongozi na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakiimba wimbo wa mshikamano katika kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.



Na Janeth Mesomapya

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu ili kuiletea tija sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka hiyo Mha. Charles Sangweni wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

“Tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha shughuli za mkondo wa juu wa petroli zinaleta chachu ya maendeleo kwenye mnyororo mzima wa mafuta na gesi asili nchini, na utendaji wetu kama wafanyakazi ndio utafanikisha hili,” alieleza.

Mhandishi Sangweni aliongeza kuwa ni vyema wafanyakazi wote wakajituma katika kutimiza majukumu yao ya kila siku huku wakiongeza ubunifu ili kuongezea thamani katika kile wanachozalisha.

Baraza hilo limeipitia na kujadili taarifa ya mapendekezo ya kuhamisha fedha kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23 kutoka idara na vitengo vya taasisi.

Aidha, baraza limejadili taarifa ya maoteo ya mapato ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2022/23, hoja za wafanyakazi na masuala mengineyo yahusuyo utendaji kazi na hali bora kwa wafanyakazi.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakisikiliza jambo wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
Viongozi na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...