Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema
Serikali inaunga mkono jitihada zote za kutangaza na kukuza lugha ya
Kiswahili ili kuhakikisha inafahamika na kuzungumzwa duniani kote.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo wakati wa utoaji Tuzo ya Kiswahili ya
Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika, tukio iliyofanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mhe. Kassim ameagiza kuwepo siku ya
Kiswahili Kitaifa ili kuithamini lugha hiyo wakati wa kuadhimisha siku
ya Kiswahili duniani, Julai 7 kila mwaka.
Pia,
Waziri Mkuu ameipongeza Kampuni ya ALAF, Tanzania na Mabati Rolling
Mills waliodhamini shindano la Fasihi ya Kiswahili kwa kengo kubwa la
kuitangaza na kuendeleza lugha adhimu ya Kiswahili duniani kote.
“Ninatoa
wito kwa Makampuni hapa nchini kuiga mfano huu kwa kuwekeza katika
lugha ya Kiswahili huku tukitambua kuwa uwekezaji wa namna hii ni muhimu
sana kwa maendeleo ya biashara zetu na taifa letu kwa ujumla”, amesema
Waziri Mkuu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohammed
Mchengerwa amesema Kampuni ya ALAF Tanzania imefanya jambo jema na
linastahili kuungwa mkono na kila mdau wa maendeleo nchini ili
kufanikisha azma ya Serikali kuitangaza na kukuza lugha ya Kiswahili
sehemu mbalimbali duniani.
“Kwa
sasa lugha ya Kiswahili ni muhimu katika ukanda wetu wa Afrika
Mashariki kwa kuwa unatuunganisha sanjari na Makabila yote yaliyopo
kwenye ukanda huu, kwa hiyo ndio maana nasema lugha ya Kiswahili ni
lugha muhimu kuitangaza na kukuza pia ”, ameeleza Mhe. Mchengerwa.
Naye,
Mkurugenzi Mkuu wa SAFAL Group, Anders Lindgren ameshukuru kwa ujio wa
wadau wote na kusisitiza kuwa Kampuni yao itaendelea kuwekeza katika
jamii ikitambua umuhimu wa jamii zinazotuzunguka.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya Washindi wa 2021, Mshindi wa tuzo ya Riwaya,
Halfani Sudy alitoa shukrani za dhati kwa waandaaji na wadhamini wa tuzo
akisema”, Tuzo hizo zimetupa jukwaa la kukutana na wadau muhimu na
kufunguka kiuchumi, hii ikiwa ni juu ya zawadi ya fedha taslim kama
washindi”
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi tuzo mshindi wa kwanza wa Riwaya,
Khalfan Sudy (kushoto) katika hafla ya utwaji wa tuzo za Kiswahili ya
Mabati - Cornell ya Fasihi ya Afrika iliyoandaliwa na Kampuni ya Mabati
ya ALAF, Tanzania hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabati ya ALAF Tanzania, Ashish
Mistry, katika hafla ya utwaji wa tuzo za Kiswahili ya Mabati – Cornell
ya Fasihi ya Afrika iliyoandaliwa na Kampuni ya Mabati ya ALAF Tanzania
tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...