Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda,Jaji Mfawidhi Kanda ya Arusha,Mosses Mzuna,wakipata ufafanuzi Kati ya moja ya Banda katika wiki ya sheria iliyozinduliwa tar 23/1/2022
 Maandamano ya wiki ya sheria yakiingia katika viwanja vya ambapo mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda .
 Mkuu wa wilaya ya Arusha akisikiliza Said Mtanda shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha waandishi wa Habari wanawake TAMWA 23/1/2022
 Baadhi ya mawakili waliodhiriki katika uzinduzi wa wiki ya sheria yaliyofanyika Mkoani Arusha 23/1/2022

 Baadhi ya wanachama wa Chama Cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA)kutoka kulia ni Ashura Mohamed,katikati ni Vero Ignatus na wakwanza kushoto ni Veronica Mheta
 Baadhi ya mawakili waliodhiriki katika uzinduzi wa wiki ya sheria yaliyofanyika Mkoani Arusha 23/1/2022
 Mwanasheria wa Jiji la Arusha,Idadi Ndabliona :Jiji la Arusha linaendelea kutoa msaada wa kisheria katika maeneo mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi



Na Vero Ignatus,Arusha


Watoa haki wametakiwa kuwa na Maadili,ili wananchi wasiwe na mashaka nao Hakikisheni watu wanapata haki zao tena kwa wakati ili waweze kwenda kuendelea na shughuli zao za Maendeleo

Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Arusha,Said Mtanda kwa wadau wa sheria wakiwemo Mahakimu kuhakikisha wanatoa haki kwa wadau wa Mahakamani ili wawe na imani katika kutatua kesi zinazofikishwa mahakamani

Mtanda ameagiza Wanasheria kutumia zaidi siku ya wiki ya sheria ili kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi inayoongoza katika Wilaya na Mkoa wa Arusha,na kuleta tija kwa Jamii nzima.Ikumbukwe kuwa haki inapocheleweshwa Ina chelewesha Maendeleo katika Jamiii.Alisema Mtanda

Alisema baadhi ya Mahakimu wanatumia fursa za kujipatia fedha kupitia kesi mbalimbali na hatimaye wananchi kukosa haki na wengine haki zao kucheleweshwa wakiwa mahabusu

Aidha wiki ya sheria imebeba kauli mbiu isemayo "Zama za Mapinduzi ya nne ya Viwanda,Safari ya Maboresho kuelekea Mahakama Mtandao" kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa sheria kikiwemo Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) pamoja na Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Alisema ni vema watoa haki wakaepuka rushwa na kutenda haki ili wadau wa mahakamani wawe na imani na mahakama katika utoaji haki na si ucheleweshwaji

"Arusha kunamigogoro mingi ya ardhi hivyo jaribuni kuitatua ikiwemo kuhakikisha mnatoa haki bila upendeleo na msiwacheleweshe wanaotaka haki kupata haki zao pia nawapongeza Tamwa mnafanya vizuri kutetea wanawake na watoto endeleeni kutoa elimu zaidi ikiwemo halamshauri ya Jiji endeleeni kutoa elimu mbalimbali katika wiki hii ya sheria ili wananchi wajue kuhusu migogoro wanayokumbana nayo wanawake na watoto"

Naye Jaji Mfawidhi Kanda ya Arusha,Mosses Mzuna alisema kupitia mahakama mtandao mwaka huu wa 2022 wameshasajili kesi 56 na wanaishukuru serikali kwa kujenga majengo mazuri ya mahakama yanayotoa huduma za kisheria kwa pamoja

Wakati huo huo, Mwanasheria wa Jiji la Arusha,Idadi Ndabliona alisema Jiji la Arusha linaendelea kutoa msaada wa kisheria katika maeneo mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi kwani wanawake wengi na watoto wanashindwa kumiliki ardhi au mali waznazoachiwa kwasababu ya baadhi ya mila kandamizi

Naye mmoja kati yawanachama wa Tamwa,Ashura Mohamed amesisitiza waandishi wa Tamwa mkoani hapa wataendelea kutoa elimu kwa wanawake na watoto wanaofanyiwa ukatili ili kuibua changamoto waanzokutana nazo na kupaza sauti ili kudhibiti ukatili kwa wanawake na watoto kupitia wiki hiyo ya sheria

Kwa upande wake Prosper Kihundwa Kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa wanyama pori akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi alisema(TAWA)wameona vyema kushiriki wiki ya sheria ili kutoa Elimu kwa wananchi watambue kuwa ni kosa kisheria kuwa na nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Aidha alisema nyara za Serikali ni nyara yeyote ambayo haijamilikishwa kwa mtu yeyote au Taasisi yeyote iliyotaifishwa kwa mujibu wa sheria ya kuhifadhi wanyama pori na.5 ya mwaka 2009.

"Nyara ni mnyamapori aliyehai au amekufa pembe,jino,kuchat,kwato,ngozi,nyama,vinyweleo,nywele,manyoya,yai au sehemu yoyote ya mnyama ikiwa ni pamoja na nyara zilizotengwezwa, vyote hivi akikutwa navyo mtu sheria inafuata mkondo wake alisema Kihundwa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...