Na Muhidin Amri,Tunduru


MRATIBU wa mfuko wa Maendeleo ya jamii nchini(Tasaf)mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira,amewaasa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini wanaopokea  ruzuku ya fedha kutoka Tasaf kuanzisha miradi ya kimkakati na biashara ndogo ndogo ili kuwaingizia kipato.

Mlimira ameyasema hayo  kwa nyakati tofauti,wakati akizungumza na wanufaika  wa mpango huo katika kijiji cha Chikomo na Chiwana kata ya Chiwana Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani humo.

Alisema, walengwa wakiwa na miradi ya kiuchumi kama ya ufugaji na mama lishe wataweza kumudu maisha yao ya kila siku bila shida, hata pale mpango wa kupokea fedha kutoka Serikalini utakapokoma(kumalizika).

Amewashauri kuanzisha vikundi vya kupeana na kukopeshana ambavyo  vina umuhimu mkubwa kwenye  familia na jamii hasa yenye kipato cha chini kupata fedha za kujikimu kimaisha na kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo.

Aidha,amewakumbusha kujiwekea akiba na kutumia fedha  hizo kwa malengo, badala ya kuzielekeza katika anasa ikiwamo ulevi na wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja  kwani tabia hiyo inachangia kuongeza umaskini katika  jamii.

Alisema, malengo ya Serikali kutoa fedha kupitia Tasaf ni kuona kila kaya ina uwezo wa kupata milo mitatu kwa siku,wananchi wapate huduma za matibabu na watoto wanaosoma wapate mahitaji ya shule na mavazi.

Akizungumzia changamoto ya walengwa kukosa kadi za Bima ya afya licha ya kuchangishwa fedha Mlimira, amewatoa hofu na kueleza kuwa tatizo hilo litakwisha kwani liko ya chini ya uwezo wake na kuwataka kuendelea kuchangia  ili waweze kupata matibabu.

Baadhi ya wanufaika wa Tasaf, wameishukuru Serikali  ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kuendelea kutoa fedha  ambazo zimesaidia  kuboresha maisha yao.

Hadija Hamis alisema, kupitia fedha za Tasaf amefanikiwa kujenga nyumba ya matofari na kuezeka bati na kuanzisha biashara ya kufuga kuku ambao unamwezesha kupata fedha za kujikimu na familia yake na kuiomba Serikali kuendelea na mpango huo.

Hata hivyo mlengwa mwingine Said Mapepe alisema,walengwa wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF)lakini baadhi yao bado hawajapa kadi za matibabu hivyo kupata usumbufu pindi wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

“walengwa tunatoa fedha kwa ajili ya kujiunga na CHF,lakini tangu tulipoanza  kuchangia mwaka 2020 hatujapata kadi  zetu za matibabu”alisema Mapepe

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji cha Chiwana Issa Simba amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa,wanaohusika ni waratibu wa CHF ngazi ya wilaya na mkoa ambao ndiyo wanaokusanya fedha kutoka kaya maskini.

Simba,amewakumbusha wakazi wa kijiji hicho kuweka akiba ya chakula kwa ajili ya matumizi ya familia zao ili kuepuka kukumbwa na janga la njaa.

Mratibu wa  mfuko wa maendeleo ya jamii(Tasaf)mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira kulia,akizungumza na wanufaika wanaopokea fedha za ruzuku katika kijiji cha Chiwana Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani humo wakati wa zoezi la malipo kwa walengwa wa kijiji hicho.
Baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini wa kijiji cha Chiwana wilayani Tunduru wakimsikiliza Mratibu wa Tasaf mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira  wakati wa malipo ya ruzuku ya fedha kwa wanufaika inayotolewa na Tasaf.

 Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini(Tasaf)mkoani Ruvuma Xsaveria Mlimira kulia akimsikiliza mlengwa wa kaya maskini wa kijiji cha Chikomo kata ya Chiwana Halmashauri ya wilaya Tunduru Ali  Wadali kuhusiana na changamoto mbalimbali  inayowakabili walengwa wa mfuko huo ikiwamo kuchelewa kwa ruzuku na kukosekana kwa kadi za matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...