Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi  la Mungu Baba, Baba Halisi akiongoza ibada ya kuliombea Taifa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Waumini wa Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiwa wameshika kalenda ya Majira     na wakati kabla ya uharibifu baada ya kutaangazwa rasmi na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KANISA Halisi la Mungu Baba lenye makao makuu yake Tegeta Namanga mkoani Dar es Salaam limefanya maombi maalumu ya kuliombea Taifa la Tanzania pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan huku likisisitiza umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote.

Maombi hayo kwa Taifa yamefanyika wakati wa Ibada maalum ya Kanisa Halisi la Mungu Baba wakati wakitagaza kurejea kenye Majira na wakati kabla ya uharibifu.

Katika kurejea huko kwenye Majira na wakati kabla ya uharibifu, Kanisa hilo limetoa kalenda yake inayotumika kuhesabu majira hayo ambayo haifanani na kalenda ya sasa inayoanzia Januari hadi Desemba, bali yenyewe inaanzia hivi na Kisleu(1), Thebeti(2), Shebati(3), Adari(4),Abibu(5), Zivu(6), Siwani(7), Tamuzi(8), Abu(9), Eluli(10), Ethanimu(11) na Buli(12).

Akizungumza mbele ya maelfu ya waumini Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi mbali ya kuelezea kurejea kwenye Majira mapya amezungumzia umuhimu wa Watanzania kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Taifa kwa ujumla ili amani na utulivu uliopo uendelee kuwepo.

"Leo hii tumekusunyika Waumini wa Kanisa hili kutoka mikoa yote ya Tanzania na nje ya mipaka ya nchi yetu,mbali ya kufanya ibada yetu maalum inayokwenda sambamba na kurejea kwenye Majira Mapya, ni vema sote tukasimama na kuliombea Taifa letu, tukamuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.Hakika Taifa la Tanzania limebarikiwa na Chanzo Halisi, "amesema Baba Halisi wakati wa kuliombea Taifa.

Amesisitiza ni lazima kumuombea Kiongozi wa Nchi kwani kupitia yeye Taifa la Tanzania liko salama na watu wake wameendelea kuwa na amani huku akitumia nafasi hiyo kueleza ujumbe wa ibada ya siku hiyo inasema hivi "Ramani mpya, jengo jipya na Maisha mapya yaliyowaingiza katika majira yasiyo na uharibifu."

Baba Halisi amewakumbusha waumini kutambua Kanisa ni moyo ulioumba kila kitu, hivyo wakiulizwa wasipapase katika kutoa majibu yake na kwamba Kanisa au taasisi kila iliyoumbwa na kujitegemea katika safu iliyokusudiwa.Aidha amesema Chango halisi anakaa ndani ya moyo wake lakini jambo muhimu ni kutenda haki.

Akifafanua kuhusu kimetokea nini mpaka wanarejea kwenye Majira na Wakati kabla ya uharibifu, Baba Halisi amesema "Si kwa mfano tena, sasa ni uhalisia wa haki.Katika mistari hii ya Mwanzo 1:27-28, mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu majira saba zilizopita.

"Katika Zaburi 8:4-6, mtu akaandikwa kuwa ni punde dogo kuliko Mungu !Pamoja na hapo bado mtu alikuwa ni kwa mfano tu sio halisi ya Mungu majira saba! suala hilo ndilo lilisababisha katika Ezekieli 32:12-13 iandikwe kuwa haki ya mwenye haki haitamsaidia.Na ilikuwa hivyo katika majira zote saba ,mwenye kupata haki hakupata haki.

"Katika majira moja halisi ambapo Chanzo cha nema a mazuri  amekuja mwenyewe aliyekuwepo kabla ya kitu chochote kuwepo, ni tofauti kabisa.Baada ya waliokusudiwa kuvushwa bonde la Uvuli wa mauti yaani kuvushwa Ufunuo 11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21  na 22 kuvushwa mto usiovukika ikiwa na maana ya Ufunuo 22:18-19; 

"na kuvushwa ulimwengu wa roho uliomeza waliotumwa wote(Efeso 2:5-8) na kuvushwa korongo la giza(2 Korintho 4:6 kutoka 20:21);kisha kuingizwa bustani mpya, sasa wamekuwa halisi kwa haki.Ukiwa uhalisia wa haki ina maana wewe siyo kwa mfano tena.Hii sasa ni zaidi ya Mwanzo 1:27-28".

Baba Halisi amesema kuwa Siyo uso mwema tena, sasa ni sura halisi ambapo amefafanua katika Ufunuo 22:3-4 iliandikwa kuwa "Hapatakuwa na laana yoyote tena.Na kiti cha enzi cha Mungu na mwana kondoo kitakuwemo ndani yake.Nao watamuona uso wake na jina lake litakuwa katika vipaji nyuso zao."

Amesema hiyo ina maana kuwa utimilifu wa Isaya 57:15 ambapo Chanzo halisi anatakiwa kuishi ndani ya kila alekusudiwa ili aonekane kwenye sura siyo tena uso.Uso wa Mungu katika majira saba yaani ukikutana na Mungu, ilimaanisha radi, ngurumo, tetemeko na umeme(Ufunuo 8:3-)









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...