Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Waziri
wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji ametoa siku tatu
kwa tume ya ushindani nchini (FCC), kutoa majibu ya kupanda kwa bei ya
vinywaji na kupotea sokoni. Pia ametoa siku saba kwa FCC, kutoa majibu
ya kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi nchini ikiwemo nondo na saruji.
Dk.Kijaji
Amesema hayo Leo wakati alipofanya ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe
kushika nafasi hiyo katika ofisi za FCC Mkoani Dar es Salaam.
Dk.
Kijaji Amesema Mje na majibu ya haraka katika ya kupanda kwa bidhaa
hizo katika kipindi hiki, hali inayopelekea changamoto kubwa kwa
wananchi.
Amesema kumekuwepo na hali ya upandishaji wa bidhaa mara kwa mara bila ya kuwepo sababu za msingi, huku FCC wakiwa kimya.
"
Hii sio sahihi, tupo kwaajili ya kulinda walaji, sasa kama hali inaenda
hivi na nyie mnakaa kimya, sidhani kama mnatekeleza wajibu wenu
ipasavyo.
Aliwataka kufanya chunguzi makini zinazotoa majibu haraka na sahihi kabla ya wananchi kupata athari.
Aliwataka
FCC kujiuliza je ni sahihi tatizo litokee kwa jamii ndio watoe majibu
au wanatakiwa kutambua changamoto mapema kupitia chunguzi zenu na
kueleza jamii njia sahihi ya kuepuka changamoto hizo
Waziri
Kijaji aliitaka FCC kutokaa kimya katika changamoto mbalimbali
zinazojitokeza hasa za upandaji wa bei ya bidhaa ikiwemo za ujenzi na
vinywaji.
" Ni vyema mkafanya chunguzi zenu vizuri kwa kina na
haraka, ilikubaini sababu yakubadilika kwa bei za bidhaa mbalimbali
sokoni kwa vipindi flani,"
Mnatakiwa kutembelea katika viwanda
mbalimbali vya uzalishaji, ilikujionea hali halisi ya uzalishaji,
kulinganisha na bei ya bidhaa zinavyouzwa sokoni.
" Mkifanya
hivyo mtaweza kubaini changamoto ya mabadiliko ya bei ilikuruhusu
majadiliano na wazalishaji juu ya kuweka bei rafiki inayoendana na hali
halisi ya maisha ya wananchi.
Alisema FCC ni moyo wa Wizara ya
Uwekezaji, Viwanda na Biashara, hivyo ndiyo inayoweza kuamua kubadilisha
kuleta maendeleo makubwa.
" Tumeaminiwa na kupewa majukumu haya
mazito, hivyo nimeamua tusongembele kama kuna mtu ambaye hataki hilo na
kutaka turudi nyuma sehemu hii sio yake atupishe," alisisitiza
Waziri
Kijaji alisema hatovumilia uzembe wowote na uvivu na kusema kuwa
anatamani kuona mwendo wa mchaka mchaka ili kutimiza malengo.
Pia aliwataka kufanya uchunguzi na kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa bora nchini zinazo endana na uhitaji wa soko huria la sasa.
"
Nivyema mkajitathimini ili kuboresha mipango yenu ili kufikia malengo
na matarajio ya wananchi. Mkumbuke mmeshikiria uhai wa wananchi kupitia
kuwalinda walaji kwa ukaguzi wa bidhaa feki hivyo endelezeni kwa juhudi
adhima hiyo," alisisitiza.
Waziri Kijaji aliwaahidi FCC
kuongezewa wafanyakazi kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi
kuajiri zaidi ya wafanyakazi 15000.
Pia Waziri huyo alimpongeza
Rais Samia kwa kumwamini na kumteua kuwa Waziri na kusema atahakikisha
anatimiza malengo ya kuaminiwa kwake kushirikiana na FCC.
Kwa
upande wake Dk. Godwin Otieno mwakilishi wa Mwenyekiti wa bodi hiyo,
alimshukuru Waziri Kijaji kwa kutambau umuhimu wa FCC nakufanya ziara
yake ya kwanza ofisini hapo toka ateuliwe na Rais Samia.
"
Tunakuahidi ushirikiano wakutosha katika majukumu yako haya.Pia
tunatambua kazi kubwa uliyo kutokana na ukubwa wa wizara hii na umuhimu
wake kwa jamii hivyo tutakuwa bega kwa bega na wewe," alisema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio alimshukuru Waziri Kijaji na kuahidi kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa.
Akieleza
kazi yao ambayo wameifanya kwa miezi sita Juni hadi disemba mwaka Jana
alisema wamefanya ukaguzi wa makontena 2831 katika bandari ya Dar ea
salaam.
Alisema makontena 258 yalikamatwa yakiwa na bidhaa bandia ikiwemo vifaa vya magari na stationari.
Mkurugenzi
mkuu alisema katika kwaka huu wamejidhatiti kutekelza majukumu yao
ikiwemo, kulinda walaji, kufanya ukaguzi wa muungano wa makampuni.
"
Wizara hii ni kiini cha ukuaji wa uchumi wa Taifa hivyo nafurahi na
kumpongeza Rais Samia kwa kuniamini na kunipa jukumu hilo kubwa"
Waziri
Mh.Dkt Kijaji alisema jukumu hilo analiweza hivyo atashirikiana na
wadau mbalimbali wakiwemo FCC ilikutimiza adhima ya Rais Samia kumteua
katika Wizara hiyo.
"Naamini inawezekana kutekeleza jukumu hili muhimu, nimeamua tufanikiwe na asiyetaka hili sio sehemu yetu"
Akieleza
sababu ya kufanya ziara yake ya kwanza FCC, alisema nikutokana na
umuhimu mkubwa wa taasisi hiyo katika Wizara yake hiyo ya Uwekezaji,
Viwanda, na Biashara
" Tume ya ushindani ni moyo wa Wizara ya
Uwekezaji, Viwanda na Biashara na mnaweza kuamua tusonge mbele au
tusiende, ila nitahakikisha tuaenda"
Dkt.Ashantu Kijaji aliwapongeza tume hiyo kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kuwalinda walaji nchini.
" Mnafanya kazi kubwa lakini niwatake muone namna ya kujiboresha ilikufikia malengo na matarajio ya wananchi"
Waziri
wa Uwekezaji Viwanda na Biashara,Dk Ashatu Kijaji akizungumza na
Waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa FCC katika ofisi ndogo
zilizopo Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...