Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Usafiri chini ya Ardhi (LATRA CCC) Leo Ngowi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana mtu mmoja kuhamasisha kwenye mitandao ya kijamii kwa madereva kwendakasi ambapo ni kinyume cha sheria ya usalama barabarani leo jijini Salaam.
*Madereva watumie taaluma zao kufuata sheria za usalama barabarani
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jami
BARAZA la Ushauri wa Watumiaji Usafiri chini ya Ardhi (LATRA CCC) limewaka abiria kutokubali mwendokasi kwani madhara yake ni makubwa pale inapotokea ajali.
Hayo ameyasema Kaimu Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Leo Ngowi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kukemea kauli iliyotolewa na abiria na kusambazwa katika mitandao ya jamii ikihamasisha madereva kwenda kwa kasi huko Wilaya Same mkoani Kilimanjaro.
Ngowi amesema kitendo kilichofanywa na abiria huyo ni makosa na kuomba vyombo vinavyohusika kumchukulia hatua kutokana na kuhamasisha madereva kwenda kasi.
Amesema madereva wanatakiwa kufuata kanuni za usalama barabarani na kufuata taaluma za udereva na sio kusikiliza abiria kwani kwenda mwendo wa kasi sio haki yao.
Ngowi amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na watumiaji kutokuwa sehemu ya chanzo kwa mwendokasi wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha Dereva anawafikisha salama kama sheria za usalama barabarani zinavyowata.
Aidha amesema kuwa watumiaji wa usafiri wanatakiwa kutoa taarifa pale wanapo ona kuna mwendokasi wa gari kwani ikitokea ajali waathirika ni wao abiria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...