Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Ambwene Sanga (34) baba wa kambo na Marko Mbilinyi (32) wakazi wa Imalilo wilayani Wanging’ombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanae Mesia Kaduma (5) na kumtupa korongoni.
Kamanda Issah amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa nan a kutarajiwa kufikishwa mahakamani huku sababu kuu ikitajwa ni chuki
“Huyu mtoto wa kambo anasoma shule ya chekechea Imalilo,alipotea na alivyopotea akawa anatafutwa mpaka serikali ya kijiji ikahusisha wanafunzi na wanakijiji ndipo mtoto huyu alipokutwa korongoni akiwa amekatwa majeraha makubwa tisa kwenye kichwa chake na wadudu kama sisimizi na siafu walishapamba mwili wake na kujipatia chakula”alisema Kamanda Issah
Issa amesema jambo la kushangaza na baba wa mtoto huyo aliungana na wananchi kutafuta mwili wa mtoto huyo wakati ni miongoni mwa waliohusika na maujai.
“Baba wa mtoto huyo amabye ni baba wa kambo naye alikuwepo kwenye msako lakini yeye ndiye aliyehusika na mauaji hayo,hii ni roho mbaya ama ni chuki huwezi kusema ni wivu wa mapanze kwasababu mwanamke aliyekuwa naye tayari alikuwa amezaa mtoto”alisema Kamanda
Kamanda amesema jeshi hilo linatarajia kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao pindi upelelezi uatakapo kamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...