Mkuu wa wilaya awapongeza, ataka iendelee kuunga mkono jitihada za Maendeleo

Mwanga.10 Februari 2022.Benki ya Mwanga Hakika Bank imetoa jumla ya madawati na meza 472 yenye thamani ya zaidi ya milioni 30 kwa shule za sekondari Wilayani Mwanga ili kukabiliana na uhaba wa madawati wilyani humo.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi 30,000,000 vitasaidia kupunguza uhaba wa viti na meza kwa wanafunzi wapatao 13,429 kutokana na ongezeko la wanafunzi 233 kwa mwaka wa masomo 2021/2022.

Kabla ya msaada huo, Wilaya hiyo ilikuwa na upungufu wa viti na meza 689 kwenye shule 10 kati ya 26 za Sekondari Wilayani humo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Mwanga Hakika, Mhandisi Ridhuan Mringo alisema lengo la msaada huo ni kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunzia.

“Benki yetu inatekeleza sera yake ya wajibu kwa jamii kwa kuangalia maeneo yenye uhitaji ikiwamo sekta ya elimu.Msaada huu wa madawati ni katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia Pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini,” alisema Mringo.

Alisema benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo ili kuhakikisha malengo makubwa ya Taifa yanafikiwa kwa asilimia kubwa.

“Benki yetu imeweza kukua kutoka kuwa benki ndogo na kuwa benki inayokuwa kwa kasi.Tunaamini ukuaji wa benki hii unatupa uwezo wa kuweza kuchangia zaidi kwenye masuala ya kijamii kama ilivyofanyika hii leo,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya aliishukuru Benki ya Mwanga kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo Wilayani hapo na kwamba itasaidia kufanikisha mipango mikubwa ambayo Wilaya hiyo imejiwekea kwa mwaka 2021/2022.

“Madawati haya yanakwenda kwenye shule ambazo tulikuwa tuna upungufu mkubwa wa madawati zaidi ya 600.Kwa ujumla tunashukuru kwa madawati haya yatakwenda kumaliza matatizo ya madawati kwenye shule za sekondari na baadaye tutageukia shule za msingi,” alisema.

Mbali na msaada huo, Wilaya hiyo imefanikiwa kujenga madarasa 50 katika shule za Sekondari ikitumia Shilingi 976,000,000 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwamo bajeti kuu Shilingi 500,000,000 fedha za UVIKO-19 200,000,000, Fedha za ndani 30,000,000 pamoja na fedha za EP4R Shilingi 237,000,000.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mwanga Hakika Bank, Muhandisi Ridhuan Mringo akikabidhi meza na viti 474 vyenye thamani ya Shilingi 30 milioni kwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga,Abdallah Mwaipaya (wa pili kushoto) kwaajili ya Shule za Sekondari Wilayani humo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga, Mwajuma Nasombe na viongozi mbalimbali wa serikali.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...