Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Vijana wa Kike waliosomea masomo ya sayansi, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeweka wazi mpango wake wa kuwapa furs ana kuajiri vijana wa kike wanaomaliza vyuo katika fani za sayansi kupitia programu yao inayojulikana kwa jina la STEM (Science, Technology, Engineering, and Mathematics).
Hatua hii inaambatana na malengo ya kimataifa ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 yanayolenga kuhamasisha ushiriki wanawake na vijana wa kike kwenye sayansi. Pamoja na hayo, mpango huu kabambe wa SBL unaendana na mkakati wa Serikali ya Tanzania ya kuongeza idadi ya vijana wa kike kwenye fani za sayansi kwa kujenga zaidi ya shule za sayansi za wasichana kote nchini. SBL imeyasema haya katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo.
Kwa mujibu was SBL, pogramu ya STEM inalenga kuajiri idadi kubwa ya vijana wa kike wanaotamani kujiunga na kampuni na watafanya kazi kwa muda wa miezi kumi na miwili wakiwa na Shahada ya Kwanza/diploma ya juu au inayolingana na shahada ya kwanza katika fani za uhandisi wa umeme, uhandisi wa kielektroniki, uhandisi wa umekanika, uhandisi wa mitambo, sayansi ya chakula na teknolojia.
Saraphina Mwamaso, msimamizi wa programu hiyo kutoka SBL alizungumza kwenye warsha iliyohudhuriwa na vijana wa kike waliopo katika fani za sayansi alisema, “tangu kuanzishwa kwa programu hii ya STEM mwaka imeshaajiri vijana kumi wanasayansi wa kike kutoka vyuo mbalimbali nchini Tanzania. Programu hii pia imewainua na kuwaelimisha vijana wa kike kupitia ushauri na mafunzo. Lengo letu ni kuboresha na kuimarisha tofauti za kijinsia katika SBL hasa katika idara ya ugavi.”
Mmoja wa wahitimu wa fani ya shahada ya elektroniki na Tehama kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam (DIT), Flora Munuo, alizungumzia uzoefu wake kama mwanafunzi wa STEM. Alisema, "ni muhimu kutambua mchango wa vijana wa kike katika sayansi kwasababu ukiwa na ujumuisishwaji mkubwa huchangia uvumbuzi zaidi. Kuna idadi kubwa ya vijana wa kike ambao tuna uwezo wa kuvumbua dhana mpya na matumizi. Ninaishukuru sana SBL kwa kutambua uwezo wangu na kunipa nafasi kwenye programu hii’.
Rukia Tezura, mhitimu mwengine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na shahada ya Uhandisi wa Mawasiliano alielezea pia uzoefu wake. Alisema, "nina imani kijana yeyote wa kike mwenye kipaji katika sayansi anaweza kufanya mambo makubwa sana. Ni lazima tuwe na ujasiri wa kuchangamkia fursa hizi ambazo zitatuwezesha kupanga safari ya mafanikio katika kupitia programu kama hii ya STEM. Nawaasa vijana wote wa kike mjitokeze na muonyeshe kile mnachoweza, ni matumaini yangu kuwa wasichana wote watayapokea haya kwa furaha’.
Halikadhalika, SBL imesisitiza kuwa mkakati wake wa muda mrefu ni kukuza vipaji vya vijana wa kike kuwa viongozi bora wa baadaye wa kampuni kupitia mafunzo mbalimbali ya kujenga nidhamu na uthamani katika kila kazi ndani ya kampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...