Na Eliuteri Mangi


Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Dada Hood inayojishughulisha na kupinga unyanyasaji wa kijinsia wameandaa Tamasha la kuichangia timu ya wanawake Twiga Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 23, 2022 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa taasisi hiyo Mkuwe Issac (Mammy Baby) amesema tamasha hilo litafanyika Machi 8, 2022 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam.

"Siku hiyo tumeipanga makusudi kwa kazi tatu ambazo ni kufanya harambee kuichangia timu ya wanawake Twiga Stars, kuzindua albamu ya 'The Orange' na kuonesha vipaji vya wanawake katika tasnia ya muziki" amesema Mkuwe.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema taasisi yake inaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta za Sanaa na Michezo.

Tamasha hilo litakalofanyika Siku ya Wanawake Duniani litapambwa na wasanii wa kike 10 ambapo wasanii wa kiume pia watakuwepo.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amewapongeza Dada Hood kwa kazi zao za kuwainua watoto wa kike hasa nia yao ya kuichangia timu ya wanawake ya Taifa Twiga Stars.

Msitha ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia sekta ya michezo kwa upande wa timu za taifa za wanawake ambazo zinaendelea kupeperusha vema bendera ya taifa kimataifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Bi Leah Kihimbi amesema Rais Samia anapenda Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo na taasisi ya Dada Hood ndiyo wamefungua milango ya mashirikiano na Serikali kwenye sekta ya Sanaa na Michezo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo kwa maslahi mapana ya taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) Somoe Ng'itu ameishukuru Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Dada Hood na kuwakaribisha wadau wengine kuendelea kuwashika mkono Twiga Stars ili waendelee kuliheshimisha Taifa kimataifa.

Katika kikao hicho na waandishi wa habari, Taasisi ya Dada Hood imesaini Mkataba wa kusambaza album ya The Orange na kampuni ya Slide Visual ambapo sehemu ya mapato yatakayopatikana yataelekezwa kusaidia timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars,



 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. What Star Wars: The Old Republic players can do is to enjoy the current game and Buy SWTOR Credits at IGGM, so as to enable themselves to get excellent results in the new expansion.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...