Na Mwandishi wetu, Mirerani
DIWANI
wa Kata ya Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Salome Nelson
Mnyawi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kuwajengea darasa jipya lililomaliza changamoto ya
mrundikano kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari
Tanzanite.
Salome
akizungumza alisema darasa hilo limemaliza tatizo la wanafunzi wapya wa
kidato cha kwanza wa shule hiyo kukosa nafasi kwenye wakati wa kusoma
kwenye shule hiyo.
Amesema
serikali ya awamu ya sita ilitoa sh20 milioni kupitia fedha za miradi
ya maendeleo ya Uviko-19 na kujenga darasa na madawati ya wanafunzi.
"Tunaishukuru
serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu mama Samia Suluhu
Hassan kwani wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wamepata nafasi na
wameingia kusoma kwenye shule hii," amesema Salome.
Hata
hivyo, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kwa kutoa sh32
milioni za miundombinu ya shule hiyo ya sekondari Tanzanite.
"Kupitia
fedha hizo tulizopatiwa na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, tumeweza
kujenga darasa jipya, ofisi ya walimu na kukamilisha vyumba sita ya
vyoo vya wanafunzi," amesema Salome.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Adam Kobelo amesema changamoto ya barabara ya shule hiyo inafanyiwa utatuzi.
Kobelo
amesema wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) wa wilaya ya
Simanjiro, unakagua na kujipanga namna ya kutengeneza barabara ya kufika
kwa urahisi hapa shuleni.
Mkuu
wa shule ya sekondari Tanzanite, Jude Mziray amewaasa wazazi na walezi
wa wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanapeleka chakula shuleni hapo
ili wanafunzi wale.
"Huwezi
kuwafundisha wanafunzi wakiwa na njaa na wakaelewa hivyo suluhisho ni
chakula shuleni, wazazi na walezi wajitahidi kwenye hilo kwani ni wajibu
wao," amesema Mziray.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...