Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ametoa onyo kwa wanasiasa kuacha kuvamia maeneo ya wazi kwa kisingizio kuwa maeneo hayo hayana wenyewe baadala yake ameutaka Uongozi wa Jiji la Dodoma ikabidhi maeneo hayo kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ili iweze kuyasimamia kwa kupanda miti
Ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati akipanda miti eneo la wazi la Iyumbu huku akishirikiana na wadau wa mazingira pamoja na wanafunzi kutoka vyuo na shule mbalimbali ambapo amesema wanafunzi na jamii zote waweke utaratibu wa kupanda miti ili kutunza mazingira.
Dkt. Ndumbaro amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wanasiasa kuvamia maeneo ya wazi ambayo yapo kisheria hivyo ameutaka Uongozi wa Jiji la Dodoma kutafuta hati ya maeneo na kisha kuyakabidhi kwa TFS ili kuyasimamia na kupanda mit
Upandaji miti huo ni muendelezo wa Wiki ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya upandaji miti ambayo ilizinduliwa Februari 7,2022 na Kitaifa itafikia kilele chake tarehe 12 Februari mwaka huu
Amesem Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na TFS Ifanye utaratibu huo na ikiwezekana maeneo hayo TFS ipewe ili yawe maeneo kwa ajili ya kupumzikia Jamii ( City Park)
'' Katika miji mingi maeneo ambayo ni ya wazi yamevamiwa kwa ajili hakuna usimamizi madhubuti, hiyo kwa Jiji la Dodoma hili ili kuifanya Dodoma ya kijani ni lazima maeneo hayo yakasimamiwa na TFS
Ameongeza kuwa TFS imekuwa ikifanya vizuri sana katika suala la kupanda miti hivyo kama Jiji la Dodoma litaamua maneo yote ya wazi wapewe TFS kwa ajili ya kuyasimamia hakika Dodoma itakuwa ya Kijani
Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro amewataka Watanzania kupanda miti katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha lengo ikiwa ni Kurejesha hali ya asili ya mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu na kuongeza kuwa upandaji miti ni kuweka mazingira safi.
.Dkt. Ndumbaro amesema kuwa lazima watanzania watumie njia hizo ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa yakijani nakuwataka wanafunzi ambao hawajapanda mti watekeleze zoezi hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mary. Maganga mara baada ya kuwasili katika eneo la wazi la Iyumbu kwa ajili ya zoezi la kupanda miti kwa lengo la kuadhimisha Wiki ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya Upandaji Miti ambayo kilele chake kitakuwa ni tarehe 12 Februari 2022.Katikati ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...