Na Seif Mangwangi,Arusha

MKURUGENZI wa Jiji la Arusha Dkt John Pima amewataka vijana wanaosimamia zoezi la anwani za makazi kutojihusisha na migogoro ya kisiasa ambayo itaweza kuibuka katika mitaa na kata watakazozifanyia kazi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha maadili ya utumishi.

Akizungumza na kundi la vijana walioteuliwa kwaajili ya kuweka anwani za makazi (post code), sanjari na kubainisha na kuweka alama na majina ya mitaa katika kata 20 zilizosalia za Jiji la Arusha , Dkt Pima amesema mchakato huo ni nyeti na unahitaji uangalifu wa hali ya juu. Tayari Jiji hilo linaendelea na zoezi hilo katika kata tano za awali.

“Nimekuja hapa kufungua mafunzo yenu lakini pia kuwaeleza mambo machache ambayo tunayatarajia kutoka kwenu, sitarajii kusikia miongoni mwenu mmejihusisha na migogoro yoyote itakayojitokeza, lolote mtakalolisikia toeni taarifa kwa msimamizi wako,”amesema.

Amesema vijana hao wanapaswa kujua kuwa kazi ya Serikali ni kazi ya siri kubwa na hivyo hatarajii mambo yasiyokuwa ya kawaida ambayo yataweza kujitokeza katika zoezi hilo yatoke nje ya viongozi wanaosimamia zoezi hilo au yeye mkurugenzi.

Dkt Pima amewataka vijana hao kufanyakazi hiyo kwa bidii ili kuhakikisha linakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na Serikali na kwamba endapo watakutana na vikwazo vyovyote watoe taarifa mapema kwa maafisa wanaowasimamia.

“Tunatarajia zoezi hili la awali litaisha ndani ya wiki mbili kuanzia kesho Februari 22, 2022, baada ya hapo mtaendelea na zoezi lingine gumu zaidi ambalo ni kuweka alama ambapo hatua hii umakini zaidi tena unahitajika na ninaamini kwa jinsi ninavyowaona mnaweza kufanyakazi vizuri sana,”anasema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Dkt Pima Jiji la Arusha linatarajia kumaliza zoezi hilo Machi mwaka huu, huku kitaifa zoezi hilo likitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Mei 2022.

Kwa upande wake msimamizi wa zoezi hilo katika kata sita ndani ya Jiji la Arusha Ernesta Moshi amesema amepokea maelekezo ya Mkurugenzi kuhusiana na maadili katika kazi hiyo na ameshatoa maelekezo kwa vijana wanaoenda kutekeleza mchakato huo kuwa makini.

Vijana watakaofanya kazi ya uandishi wa anwani za makazi walimsikiliza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...