Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi leo Februari 11, 2022 amezindua Tamasha la Muziki la Serengeti la mwaka huu jijini Dar.

Akizindua Tamasha hilo mbele ya Waandishi wa Habari, Dkt. Abbasi amesema tamasha la mwaka huu linakusudia kutangaza Utamaduni na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

Aidha amesema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya wasanii 50 na litashirikisha wasanii wa lebo zote.

Ameongeza kuwa wasanii wakongwe na wachanga watashiriki ili kuleta ladha tofauti tofauti.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Fareed Kubanda amepongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatumia wasanii kutangaza miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Serikali ya Tanzania ndiyo Serikali pekee duniani ambayo inawatumia zaidi wasanii katika utekelezaji wa kazi za Serikali". Amefafanua Kubanda

#MADEINTANZANIA
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi (kushoto) akiwa pamoja na msanii mkongwe wa kizazi kipya Faridi kubanda (FID Q) wakionesha nembo ya Tamasha la Muziki la Serengeti la 2022 ambalo litafanyika mwezi Machi mwaka huu jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akieleza mikakati ya uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 11,2022 katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam

Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda (FID Q) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam


Mkutano wa Waandishi habari ukiendelea wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo adhimu litakalofanyika Mwezi Machi jijini Dodoma. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...