Na Mwandishi Wetu

WAKAZI  wa Buza Kanisani, Mtaa wa Amani, wamelamikia mfanyanya biashara kwa kujenga ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi (residentional) , jambo linalosabisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa njia ya sauti kutokana kelele zinatoka katika ukumbi huo.

Wanamshtumu mfanyabiashara huyo waliyemtaja kwa jina moja la  Shayo kwa kuvunja sheria za matumizi ya ardhi kwa  ukumbi wa sherehe na bar kubwa  kwenye la eneo ambalo limepimwa na mamlaka za Serikali kwa ajili ya makazi, na sio biashara.

"Tunashindwa kulala usiku, watoto wetu wanashindwa kujisomea usiku kwa kelele na ghasia zinasababishwa na ukumbi huu," amesema Mika Moza ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

"Serikali imetumia fedha nyingi za walipa kodi kupima maeneo haya ya makazi, iweje leo mtu anabadilisha matumizi ya ardhi kiholela kwa kufanya biashara kama hii yenye athari kubwa kwa mazingira kwa njia ya sauti/ kelele, alafu serikali ya mtaa iko kimya," amesema mkazi mwingine, Kulwa Muga

Wakazi wamedai kuwa wamewasilisha malalamiko yao (kwa maandishi) kwa Ofisa mipango miji- Manispaa ya Temeke tangu Mwaka 2013, lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

"Mfanyabiashara huyu ni mbabe na kwa sababu ana  pesa kiongozi wa serikali ya mtaa, baadhi ya maafisa wa mipango miji -Temeke Manispaa hawawezi kudhibiti jambo hili, hali inayosababisha hadha kubwa kwa wakazi wa eneo hili," amedai mkazi Moza Mrope.

Wakiendelea kueleza wakazi hao wamedai  mfanyabishara  baada ya kuvunja sheria kwa miaka zaidi ya ya tisa, hivi karibuni maofisa mipango miji -Temeke manispaa wamemshauri kubadilisha matumizi ya kiwanja hicho No. 686, Kitalu E, kutoka makazi kwenda biashara, jambo ambalo wamedai nu uvunjifu wa sheria za mazingira.

"Kumruhusu abadilishe matumizi ya kiwanja kutoka makazi kwenda biashara, ni kosa kwa sababu maeneo haya yamepimwa kwa ajili makazi, na si biashara...Manispaa wakiruhusu jambo hili watakuwa wamebariki rasmi uchafuzi wa mazingira na uvunjaji wa sheri za mazingira, bila kujali athari za kelele na uchafu huu mkubwa wananchi walio wengi.

Alipohojiwa, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani  Omary Katoto amesema "Sio wakazi wote wanalalamika kuhusu jambo hili, ninachofahamu mimi ni kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya mfanyabiashara huyo na mtu mmoja katika eneo hilo."

"Miaka kama mitatu iliyopita walipelekana Polisi, walitishiana maisha sijui, lakini niliitwa kama Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa, nikawasihi Polisi watuachie jambo lile tukalisuluhishe kirafiki kama wa mtaa mmoja, walikubali ...tulikaa chini tuongea na pande zote mbili, tukamaliza. Leo hii nashangaa kuone jambo hili nimeibuka tena.".

Alipotafutwa, Ofisa Ardhi Wilaya ya Temeke Salumu Ali, amesema “Njia rahisi kwa wakazi hao ni kupeleka malalamiko yao kwa maandishi kwa Mkurugenzi wa Manispaa, ili kuweka pingamizi la kuzuia mabadiliko ya matumizi ya ardhi ambayo Bw. Shayo, amepanga kuyafanya kutoka Makazi kwenda biashara.”

“Kama mamlaka, tutapokea maoni na mapingamizi ya wananchi hao, na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za maswala ya Ardhi. Hilo ndo naona kama suluhisho kwa wakazi hao wanaolalamika.”

Alipotafutwa kupitia simu yake na mkononi mfanyabiashara alipokea lakini akapokea na kusema tutaongea lakini baada ya hapo hakupokea tena simu licha ya kuendelea kutafutwa.Hata hivyo Mwandishi wa habari hii ataendelea kumtafuta ili kupata maelezo yake yatakayosaidia kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya wananchi hao.

Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Amani-Buza Omary Katoto akiwa ofisini kwake alipokuwa akifafanua madai ya baadhi ya wananchi kuhusu kulalamikia kujengwa ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...