Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WATANZANIA
wameshauriwa kuifanyisha miili yao mazoezi kama sehemu mojawapo ya
kukabiliana na kujiepusha na magonjwa yasiyoambikiza huku wakielezwa
hakuna njia ya mkato ya kupunguza mwili.
Ushauri
huo umetolewa na Dk.Grace Moshi kutoka Idara ya Kinga Kitengo cha
Huduma za Lishe Wizara ya Afya alipokuwa akichangia mada iliyokuwa
inazungumza umuhimu wa ufanyaji mazoezi na kubadilisha mtindo wa maisha
ambao unatajwa kama moja ya sababu ya kuongezeka kwa magonjwa
yasiyoambikiza nchini.
Akifafanua
zaidi kwa washiriki wa mkutano ulioratatibiwa na Shirikisho la Vyama
vya magonjwa yasiyoambikiza Tanzania( TANCDA) kwa lengo kuwasilishwa
muhtasari wa Sera juu ya lishe na kushughulisha mwili Dk.Grace Moshi
ameeleza ni jinsi gani unatakiwa kupunguza mwili bila kuathiri mfumo wa
mwili.
"Ni
muhimu kuufanyisha mwili mazoezi na unapoufanyisha mazoezi hakikisha
inakwenda sambamba na masuala ya ulaji, kwanza unapokula hakikisha
kwamba unachoma 'Carlolis' ambazo umezipata na kiukweli hakuna njia ya
mkato , wewe umejenga mwili kwa muda mrefu halafu unataka siku moja
uamke ukute umekonda ni kitu ambacho hakiwezekani.
"Wengi
wetu tunadanganyana na inafika mahali tunaacha kula unashindia maji tu
,ni kwamba hapo unatengeneza tatizo jingingine kwasababu mwili jinsi
ulivyo ili mifumo yako yoote ifanye kazi vizuri inatakiwa kuwa na kiasi
cha virutubisho ambazo mwili unatakiwa upate kila siku ili mifumo iweze
kujengeka vizuri.
"Ikitokea
umekosa kitu tayari mwili unaanza kuleta shida,utafika mahali utaanza
kuambiwa damu yako imepungua kwasababu kuna virutubisho hukuvipata
vizuri mwilini , utafika mahali utaona mifumo inaanza kukataa , wengine
tunafika mahali si unaona hata sasa hivi heshima inakuwa haipo,saa
zingine ukiacha matatizo mengine pia na hizi staili na ulaji wetu
unachangia.
"Tunakosa
vile virutubisho vya msingi kwa ajili ya kuufanya ule mfumo ufanye kazi
vizuri,kwa hiyo ukifika mahali unataka kuupunguza mwili kwa haraka
kwamba nimeamua sili ila nakunywa maji ujue kabisa unakoelekea
utapunguza baadhi ya virutubishi na wewe utaona mwili umepungua lakini
unatengeneza madhara mengine mwilini,"amesema Dk.Grace.
Ameongeza
kuwa kwa hiyo sio sawa na kwamba Kama unajua mwili umeujenga kwa muda
mrefu hivyo hata kuupunguza kwake itachukua muda, hivyo unachotakiwa ni
hakikisha unachoma Carlolis wakati unakula chakula ambacho kiko
balansi."Balansi kwa maana ya kupata chakula chenye virutubisho vyote
vinavyohitajika mwilini kwa ajili ya kufanya mifumo yako ifanye kazi
mwilini vizuri."
Kuhusu
mazoezi amesema walio wengi wanakosea."Unakuta inapigwa kampeni ya
mazoezi sawa, tunakimbia Viwanja vya Leaders , tunafanya mazoezi ya
nguvu ,unajua mwill unatabia moja ukichoma zile Carlolis halafu
ukaziongeza kwa nguvu mwili unaongezeka kwasababu si umetengenezwa
nafasi ,kwa hiyo nafasi yote inajaziwa.
"Kwa
hiyo utaona umefanya mazoezi lakini ndio unatengeneza mwill
zaidi.Lakini tunapiga kampeni tunakwenda Leaders Jumamosi tunakimbia
weee tukimaliza pale pale pembeni kuna mgaha wameweka chapati tatu na
supu yenye mafuta ,kwa hiyo unatoka pale umeshachoma Carlolis vizuri ...
"Lakini
unakwenda kuharibu zaidi kwasababu umetengenezwa nafasi katika mwili
halafu umeenda kujazia yaani umeharibu zaidi kwa hiyo unajikuta hata
yale mazoezi hayakusaidii,kwa hiyo mazoezi lazima yaende sambamba na
namna unavyokula."MWENYEKITI
wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasioambukiza (TANCDA) Prof.
Andwer Swai akitoa mada ya ugonjwa wa kisukari kwa washiriki wa mkutano
wa kuwajenga uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...