Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
-"Katika
hali ya uandikishaji inayoendelea,Kibaha Mjini mpaka kufikia
imeandikisha jumla ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 3,987 sawa na
Asilimia 88.3 ya maoteo ya Wanafunzi 4,514.
Aidha,wavulana
walioandikishwa ni 2011 ambayo ni asilimia 88.7 ya malengo ya
kuwaandikisha 2,266 huku wasichana wakiwa ni 1,976 sawa na Asilimia
87.9 ya malengo ya kuwaandikisha 2,248.
Bado uandikishaji unaendeleaje kwa mujibu wa taratibu zilizopo"Eng.Mshamu Munde Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kibaha
"Kwa
upande wa Elimu ya Msingi,Kibaha Mji inatarajia kuandikisha Wanafunzi
5763.Mpaka Februari 10,2022 Wanafunzi 5519 sawa na Asilimia 95.77
wameandikishwa.
Katika
idadi hiyo wavulana ni 2826 sawa na 101.4 asilimia na wasichana ni 2693
ambayo ni 95.77 asilimia ya malengo ya wanafunzi 2977.Uandikishaji
unaendelea....Eng.Mshamu Munde Mkurugenzi Kibaha Mji.
"Kwa
upande wa Elimu ya Awali,Kibaha Mji mpaka Sasa imeandikisha jumla ya
Wanafunzi 2,530 sawa na Asilimia 68.6 kati ya maoteo ya watoto
3,687.Kati yake wavulana ni 1,306 ambayo ni asilimia 71.8 ya watoto
1,822 wanaotarajiwa na Wasichana ni 1224 sawa na asilimia 65.63 ya
matarajio ya Watoto 1865.
Aidha,uandikishaji huu umehusisha wenye mahitaji maalum na unaendelea mpaka Mwezi Machi,2022" Eng.Mshamu Munde,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...