Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU
Wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri amemuagiza ofisa mipango miji na
kamati ya huduma za jamii kujipanga kutenga maeneo kwa ajili ya
wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo machinga ,wauza mitumba na wenye
bidhaa za kusindika, ili kuondoa malalamiko na migogoro ambayo
inajitokeza.
Aidha
amewataka waliohodhi maeneo makubwa na taasisi mbalimbali pasipo
kuyaendeleza wayaendeleze na wale watakaoshindwa taratibu zitachukua
mkondo wake wapokonywe.
Akizungumzia
katika kikao cha bajeti Cha mapendekezo ya makadirio ya mapato na
matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo cha Halmashauri ya Mji wa
Kibaha, Mkoani Pwani, Sara alieleza , Kuna kila sababu ya kuyapangia
makundi hayo maeneo yao rasmi .
"Kundi
kubwa ni la vijana ,wanahangaika kujituma na shughuli ndogondogo lakini
wanajikuta hawana Mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao, ili
kuepukana na haya mipango miji wekeni maeneo machinga wajulikane wako
wapi, wenye bidhaa za kusindika tunazipata wapi kuliko ilivyo Sasa ,Mji
huu Ni mkubwa Lazima tujipange uwe wa kisasa "alifafanua Sara.
Hata hivyo, Sara aliitaka Halmashauri ya Mji huo, kudhibiti vyanzo vya mapato na kuongeza makusanyo ili bajeti ilete matokeo.
"Rais
Samia Suluhu Hassan ,anategemea kuona matokeo ya fedha za Serikali
naipongeza Halmashauri hii kwa kusimamia fedha mbalimbali zinazoletwa ,
fedha hizi zinakuja kwa mkupuo na zinakuja kwa maelekezo ,zinahitaji
usimamizi mzuri"alisema Sara.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mshamu Munde alisema ,yapo maeneo ya
wafanyabiashara ndogondogo lakini tatizo ni udhaifu wa miundombinu ya
maeneo hayo na kuongeza maeneo yaliyo katika mpango.
Alibainisha
kwamba , yapo maeneo Loliondo, Mailmoja na pia maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya uwekezaji ,Lakini Sasa wanaelekeza mipango hiyo kuitanua kwa
Lengo la kuwapeleka wafanyabiashara ndogondogo pia eneo la Kidimu,
mkombozi na Lumumba .
Akielezea
bajeti,alisema imejielekeza kutatua changamoto za kijamii, katika
huduma za afya ,sekta ya elimu na kufungua miundombinu kwenye mitaa.
Alisema
,upande wa madarasa kwasasa Kuna unafuu ,na wamepanga kuelekeza
kutengeneza vyoo na madawati kwa wakati huu, na shule kongwe kuendelea
kuzikarabati madarasa 26 katika shule sita .
Munde
alieleza kwamba ,Kama Halmashauri imejipanga kuongeza kukusanya
makusanyo zaidi ya miaka ya nyuma na kudhibiti mianya ya wizi .
Awali
akisoma taarifa ya mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya
kawaida na miradi ya maendeleo,makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji
Kibaha,Selina Wilson alisema makadirio 2022-2023 inakadiria kukusanya
Bilioni 45.832.4 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
"Kutoka
mapato ya ndani tunategemea kukusanya Bilioni 4.321.184.9 na ruzuku
kutoka Serikali kuu tunategemea kupokea Bilioni 41.511.305.974.51 kati
ya fefha hizi mishahara ni 31.975.459.680, matumizi mengine 0C na miradi
ya maendeleo"alisema Selina.
Wakichangia
bajeti hiyo, diwani wa Pangani Agustino Mdachi alisema ,bajeti ni
nzuri, yenye kulenga kata zote Lakini haitoleta matokeo endapo fedha za
makusanyo zitakuwa haziridhishi kwani bajeti itabaki katika makaratasi.
Mdachi alitaka ,wote Kuwa wamoja kusimamia makusanyo ya mapato kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ili kuongeza mapato.
Nae
diwani wa Tangini ,Mfalme Kabuga alieleza bajeti ipo vizuri, Lakini
alimuomba nguvu kutatua changamoto ya ukosefu wa shule ya msingi na
Sekondari katika kata hiyo .
Kabuga
alisema ,hiyo ni kata iliyopo kwenye kitovu Cha Mji huo Lakini haina
shule ya Sekondari suala ambalo linahitaji kukusimamiwa kwa maslahi ya
watoto wa kata hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...