Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tarehe 08/02/2022 imekabidhi pikipiki mbili, (02) kwa Maafisa ugani wa Kata ya Mtipwili na Kingerikiti ili kuboresha utendaji kazi kwa kuwahudumia wafugaji,Makabidhiano yaliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa.

Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas, amewataka Maafisa ugani hao kutumia Pikipiki hizo, kwa lengo lililokusudiwa na Serkali hasa kwa kuwahudumia na kuwafikia kwa wakati, wafugaji kwa kutoa elimu ya ufugaji na ushauri wa ufugaji wa Kisasa ili kukuza kipato cha wafugaji, na kuacha mara moja tabia ya kutumia pikipiki hizo, kwa maslahi yao binafsi kwa kuwa pikipiki hizo zimeletwa kwa lengo la kuwahudumia wafugaji.

Ameongeza kuwa kuna baadhi ya Wautumishi wa umma wamekuwa na tabia ya kutumia mali za serikali kwa kuazimisha,marafiki zao au kukodisha na kujipatia mapato binafsi,hivyo amewataka watumie kutatua changamoto za wafugaji.

“Rai yangu kwenu pikipiki hizo zikatumike kwa yale makusudio ya Serikali, ambayo imeletwa, isiwe ni chanzo cha kutafuta bodaboda na mambo yenu ambayo sio tija, wafugaji wengi wanahitaji Elimu ya Ufugaji kwa hiyo nendeni mkazifanyie kazi vizuri,najua kuwa kata zenu ni kubwa na zina wafugaji”.

Kwa Upande wao maafisa ugani wa kutoka kata hizo wamesema watatumia pikipiki hizo kuboresha utendaji kazi wa kwa kuwa awali walikuwa na changamoto ya Usafiri ambayo iliwafanya kutowafikia wafugaji kwa haraka.


Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kanali Laban Thomas akikabidhi pikipiki mbili kwa maafisa ugani wa Kata ya Mtipwili na Kingerikiti walayani Nyasa,


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...