Na Mwandishi Wetu, Moshi
MBIO za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2022 zilizokuwa zinasubiriwa kwa hamu sasa zimewadia huku Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa Majaliwa akitarajiwa kuwaongoza maelfu ya wakimbiaji na washangiliaji kuadhimisha mmiaka 20 ya mbio hizo.
Akizungumza katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU) alisema maandalizi yote yamekamilika tayari kwa mbio za kesho.
“Tumeshakamilisha maandalizi yote na tunamtarajia Waziri Mkuu leo hii tayari kwa maadhimisho ya miaka 20 ya mbio hizo. Hili ni tukio kubwa,” alisema.
Mbio hizo zitajumuisha Km 42 za Kilimanjaro Premium Lager, Km 21 za Tigo and Km 5 za Grand Malt. Waziri Mkuu na msafara wake wanatarajiwa kushiriki mbio za Km 5.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Irene Mutiganzi alisema wanajivunia kudhamini mbio hizo kwa miaka 20 sasa. “Tumewaandalia mambo mengi mazuri ikiwemo mbio zenyewe, burudani ya aina yakke na pia bia za kutoshaza Kilimanjaro Premium Lager,” alisema.
Mbio hizi zilitanguliwa na maonesho ya aina yake maarufu kama ‘The People’s Expo’ ambayo yamefanyika kwa siku tatu kuanzia Alhamisi na kuwajumuisha wadhamini wa mbio hizo na makampuni mengine.
Mji wa Moshi ytayari umefurika huku mjimzima ukiwa umepambwa na rangi za Kilimanjaro Premium Lager, Tigo and Grand Malt. Maeneo ya starehe na sehemu za kulala wageni zimejaa huku washiriki wengine na washangiliaji wakiendelea kumumunika katika mji huo.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...