Nzunda
ametoa wito huo (03.02.2022) Mkoani Morogoro wakati akizungumza na
Bodi ya wakala hiyo na Maafisa wasimamizi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya
mifugo kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
"Anzisheni
mifumo imara ya usimamizi na uwajibikaji, huu utendaji wa kuamka
asubuhi unaenda kazini kama kawaida, umepitwa na wakati, unachelewesha
maendeleo, kwasasa tuanze kupimana kwa Mikataba ya utendaji kazi ili
tuanze kuona utendaji wa kila mmoja wetu jinsi anavyotekeleza majukumu
aliyopewa, kama umefanikiwa, sawa, na kama amekwama tatizo ni nini mpaka
umekwama? hii itatupa nafasi ya kuhoji kama unastahili kuendelea na
nafasi uliyonayo. alisema Nzunda"
Nzunda
amesisitiza kuwa Serikali inahitaji kuona matokeo chanya kupitia Sekta
ya Mifugo kwa kuimarisha na kusogeza huduma kwa wananchi ikiwemo
kuendelea kupanua wigo wa huduma za ugani kwa wafugaji ili kuondokana na
ufugaji wa mazoea usioleta tija kwa wafugaji walio wengi.
Ameongeza
kuwa Taasisi hiyo ni muhimu itekeleze jukumu la kuwafikia wafugaji kwa
kutumia rasilimali kidogo waliyonayo ili kuleta matokeo makubwa.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya wakala hiyo Prof. Malongo Mulozi, amesema kuwa
LITA wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa
usafiri wa kuwapeleka wanafunzi katika masomo ya Vitendo pamoja na
kuwafikia wafugaji.
Aidha,
ametaja changamoto nyingine kuwa ni uchakavu wa miundombinu ya
kufundishia na uhaba wa nyumba za watumishi ambapo alibainisha kuwa
pindi fedha itakapopatikana ukarabati na ujenzi wa nyumba hizo utaanza
mara moja.
Vile Vile
Prof. Mlozi amesisitiza kuwa pamoja na uwepo wa changamoto hizo, moja ya
mikakati ya Taasisi hiyo ni kuzalisha na kuandaa vijana wenye uwezo wa
kujiajiri kupitia Sekta ya Mifugo na kwamba kila kituo kina mradi wake
wa mapato kulingana na hali ya mazingira kilipo.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Dkt. Pius Mwambene amesema
kuwa majukumu makubwa ya Taasisi yake ni pamoja na kutoa mafunzo ya
muda mrefu na Mfupi, Kutoa huduma za Ushauri wa kitalaam wa Mifugo,
kufanya tafiti na tathimini pamoja na kuzalisha na kutunza Mifugo ya
kufundishia.
Dkt.
Mwambene amesema kuwa kwasasa vyuo hivyo vinawanafunzi zaidi ya 4,000
ukilinganisha na wanafunzi 700 waliokuwepo wakati wanaanza mafunzo hayo
miaka kumi iliyopita, na kwamba Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)
imeendelea kuhimiza kufanyika maboresho katika miundombinu ikiwa ni
pamoja na kusimamia ubora wa wanafunzi wanaohitimu katika vyuo hivyo.
Pia
Dkt. Mwambene ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuingia
ubia na wakala hiyo ili kusaidia uwekezaji wa mafunzo kwa wanafunzi
hao.
Mazungumzo baina ya
Nzunda na Watendaji wa Wakala hiyo yalienda sambamba na makabidhiano
ya magari mawili aina ya "Toyota Double cabin" kwa ajili ya kurahisisha
utendaji kazi kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...