MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka wadau wa madini kuzingatia sheria za utunzaji wa mazingira wakati wa uchimbaji, uchenjuaji na uchakataji wa madini.

Ameyasema hayo leo Wakati wa kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini uliofunguliwa leo Februari 22, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mpango amewakumbusha wachimbaji wa madini wakubwa na wadogo kuzingatia sheria za usimamizi wa mazingira Kwasababu uchimbaji wa madini kwa kiwango chochote unaenda sambamba na uharibifu wa mazingira.

"Wawekezaji wote mnao wajibu wa kuhakikisha kuwa shughuli zenu za uchimbaji, ujenjuaji na uchakataji wa madini zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria na taratibu ili tuweze kunufaika kikamilifu na madini yetu." Amesema Dkt. Mpango

Aidha amewataka wawekezeji wakubwa kuzingatia matakwa yanayoendana na tathmini ya athari za mazingira katika jamii na kuzingatia misingi ya uzalishaji endelevu na matumizi ya mbinu bora za uzalishaji na teknolojia rafiki kwa mazingira.

Dkt. Mpango amewaasa wawekezaji pamoja na wachimbaji kutojihusisha na ajira za watoto na badala yake waongeze juhudi hasa katika kuhamasisha, kukuza uelewa na kujenga uwezo wa jamii na wachimbaji wadogo hususani wanawake kupitia wataalamu walionao.

Licha ya hayo amezikumbusha kampuni zote zinazowekeza kwenye sekta ya madini zihakikishe zinatekeleza ipasavyo matakwa ya kisheria ya kuandaa mipango ya utunzaji wa mgodi kwa kuweka hati fungani ya urekebishaji wa mazingira.

Kwa upande wa Taasisi za kifedha na Shirika la Madini (STAMICO), Dkt. Mpango amewaomba wabuni namna bora ya kuwawezesha wachimbaji wadogo ili waweze kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo.

Hivyo amewaomba wawekezaji wakubwa kuendelea kuboresha uchumi wa wananchi katika maeneo yenye migodi kwa kutoa fursa za ajira katika migodi na kujenga urafiki na jamii inayowazunguka ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina ameiomba Serikali kuanzishwa kwa mifuko ya wachimbaji wadogo wadogo wa Madini na Benki ya Kuu Tanzania (BOT) iweke fedha kwaajili ya mfuko huo.

Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini ulihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Burundi, zimbabwe, Comoro, Sudani, Sudani Kusini, Libya pamoja na wachimbaji wa madini wadogo na wakubwa wa hapa nchini zaidi ya 1200.

Mkutano huo umedhaminiwa na Kampuni ya Uchimbaji madini ya Barrick, Twiga Minerals Corporation limited, AngloGoldAshandti, Geita pamoja na Gold Mine Tanzania.





Waziri wa Madini, Dkt. Dotto Biteko kulia akiwa katika  Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini unaofanyika leo Februari 22, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango
akizungumza na Waziri wa Madink Wakati akitembelea Mabanda ya maonesho kabla ya kuingia kwenye  Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini uliofanyika leo Februari 22, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya wachimbaji wadogo na wakubaa wakiwa katika mkutano wa kimataifa katika sekta ya madini  uliofanyika leo Februari 22, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...