MKUU wa Wilaya ya Songwe Simon Simalenga amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara yenye kipande cha urefu wa kilomita 7 kutoka Kata ya Kanga kwenda Kata ya Ifwenkenya ambayo inajengwa na Mkandarasi Elimak Engineering CO. LTD na ujenzi unaendelea vizuri.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya ya Wilaya ya Songwe CPA Cecilia Kavishe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, MENEJA wa TARURA MKOA wa Songwe Kaka Kilian Haule, Meneja wa TARURA wilaya ya Songwe Eng. Yusuph Shabani, Kaimu DAS Ndugu Chesko Mbilinyi na Viongozi wengine wa Wilaya.

Akizungumza akiwa kwenye ziara hiyo Simalenga amesema kimsingi wananchi wa Wilaya ya Songwe wamejawa na moyo wa shukrani kutokana na ongezeko la fedha za Barabarabara kutoka Sh.milioni  640 walizokuwa wakipewa mpaka kufikia Sh. Bilioni 2.84 katika kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan.

Aidha amesema baada ya kazi ya ujenzi wa Mitaro unaendelea sasa, kazi itakayofuata ni kumwaga kifusi kwa urefu huo wa kilomita 7 kisha Mkandarasi atahamia Barabara ya Kata ya Galula, Chang’ombe mpaka Mbuyuni yenye urefu wa kilomita 6.

“Mpaka sasa kazi imeshafanyika kwa asilimia 25 ambapo Mkandarasi huyu anaendelea kutumia fedha zake. Ikumbukwe kwa mujibu wa Mkataba kazi hii inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 8,"amesema Simalenga.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...