WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent BASHUNGWA amesema mpango wa elimu bila malipo umeleta fursa ya upatikanaji wa elimu kwa kuongeza uandikishaji wa wanafuz.
Waziri BASHUNGWA ameyazungumza hayo leo February 11, 2022 wakati wa utoaji tuzo za ubora wa taaluma kwa shule za msingi na Sekondari Tanzanja zilizofanyika katika ukumbi wa chuo cha Biblia, jijini Dodoma.
"Katika mwaka 2016, jumla ya wanafunzi 2,670,125 waliandikishwa, kati ya hao wanafunzi 917,137 wa elimu ya awali, 1,386,592 wa darasa la kwanza na wanafunzi 366,396 wa kidato cha kwanza. Kwa mwaka 2022, jumla ya wanafunzi 3,046,919 wameandikishwa, kati ya hao wanafunzi 1,123,800 ni wa Elimu ya Awali sawa na asilimia 82, wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,352, wanafunzi 1,454,544 ni wa darasa la kwanza sawa asilimia 91, na wanafunzi 664,698 wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,747, wanafunzi 664,698 wa kidato cha kwanza wameripoti shuleni, sawa na asilimia 73.2 ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka 2022, wakiwemo wanafunzi 679 wenye mahitaji maalum."- Amesema BASHUNGWA.
Tuzo hizo zinazotolewa kwa Mikoa, Halmashauri, Walimu na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, katika taaluma kwa mwaka 2021 na Kauli mbiu isemayo kuwa “Uboreshaji wa Ufundishaji na Ujifunzaji shuleni ni chachu ya kuongeza kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi”
BASHUNGWA amesema inathibitisha maelezo ya hali halisi iliyopo sasa, katika Sekta ya Elimu, na ametoa
maelekezo na kusisitiza mambo muhimu yafuatayo; -
1. Kuhakikisha mnafuata sheria, miongozo na taratibu katika usimamizi wa sekta ya Elimu ili kufikia malengo ya Serikali.
2. Kuhakikisha mnasimamia vizuri miradi yote, inayotekelezwa katika maeneo yenu, ili kuwa na miradi yenye viwango, ukilinganisha na thamani ya fedha.
3. Kuhakikisha majengo yote ya Serikali, ikiwemo mali za shule vinatunzwa vizuri, ili kuweza kudumu kwa miaka mingi na kutumika na vizazi vijavyo.
4. Kuhakikisha mnakuwa kiungo kizuri, kati ya viongozi walioko katika maeneo yenu na jamii, jambo ambalo litawawezesha kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi. Wapo baadhi yenu hawana mahusiano mazuri na jamii, hivyo kukwamisha utekelezaji wa baadhi ya shughuli za serikali.
5. Kuhakikisha mnandaa motisha kwa walimu, na wanafunzi ili kujenga ari ya ushindani, wakati wote wa kutekeleza sera ya elimu nchini.
6. Kuhamasisha jamii iweze kutoa chakula kwa wanafunzi wote.
Aidha Bashungwa amesema SERIKALI imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika shule za msingi na Sekondari Nchini.
Kwa mwaka 2021 ufaulu katika kumaliza elimu ya msingi umefikia 82.97%, mtihani wa kumaliza kidato cha nne umefikia 87.30% na kidato cha sita 99.62%.
BASHUNGWA alimaliza kwa kuwaahukuru walimu, wazazi, na walezi kwa kuongeza na kuimarisha ufaulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...