Na Mwandishi Wetu,Shinyanga
KUKOSEKANA kwa upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania kumetajwa kuwa moja ya chanzo cha mauaji ambayo yametokea katika maeneo mengi hapa nchini katika siku za hivi karibuni.
Hayo yameelezwa juzi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ongezeko la matukio ya mauaji ambayo yametokea hivi karibuni katika maeneo mengi hapa nchini.
Mgeja amesema katika uchunguzi wake amebaini matukio mengi ya mauaji ni yale yanayohusiana na wivu wa kimapenzi kati ya wapendanao na uwaniaji wa mali ndani ya familia ambapo baadhi ya watoto wamekuwa wakiwaua wazazi wao kwa lengo la kupata m
ali.
Akifafanua amesema ukichunguza kwa undani ni wazi kwamba mauaji hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na watu kutokuwa na upendo miongoni mwao, hasa ikizingatiwa wanaofanya mauaji hayo ni watu wa karibu kabisa ndani ya familia.
Ameongeza iwapo watanzania watadumisha upendo na mshikamano miongoni mwao kama walivyo viumbe wengine mfano wa ndege aina ya njiwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya mauaji yanayotokea hivi sasa hapa nchini.
“Watanzania tudumishe upendo na mshikamano kama walivyo viumbe wengine mfano wa ndege aina ya Njiwa, maana tusipokuwa na upendo ni wazi tunaweza kutoana roho kwa mambo madogo madogo ambayo kama upendo na mshikamano vingekuwepo yasingetokea.
“Nichukue fursa hii kuwaomba watanzania wenzangu, tujenge utamaduni wa kupendana na kuhurumiana pale mmoja wetu anapopatwa na matatizo asaidiwe badala ya kuchekwa, na kama ni suala la mahusiano ya kimapenzi, basi busara itumike katika kutatua changamoto zinazojitokeza, badala ya kukimbilia kutoana roho,” alieleza Mgeja.
Ametoa mfano wake yeye mwenyewe ambaye amekuwa na tabia ya kuwakirimu kwa kuwapa chakula ndege aina ya Njiwa ambao kwa kipindi kirefu na wao wameonesha upendo kwake kutokana na kwenda nyumbani kwake kila asubuhi na kukaa naye pamoja japokuwa wao si binadamu wenzake. “Ukiacha wanadamu hata
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...