MUWEKEZAJI wa kiwanda cha kukata, kung’arisha na kuuza mawe ya asili aina ya Marbo na Granites jijini Mbeya ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mipango, mikakati na jitihada za kizalendo kwa kuinua uchumi wa nchi hii ikiwemo uchumi wa viwanda.

Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya Marmo E Granito Mines (T) Limited ikiwa ni sehemu ya mafunzo yaliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuwajengea uwezo wa kuandika kwa usahihi masuala ya Uchumi, Biashara na Fedha, Afisa Utawala na Rasilimali Watu wa kiwanda hicho, Bw. Brinton Kulinga alisema mipango ya serikali imesaidia kukifanya kiwanda hicho kuendelea kupiga hatua tangu kilipoanzishwa hadi hivi sasa.

Alisema kiwanda hicho kilichoko eneo la viwanda Iyunga jijini Mbeya awali kilikuwa kidogo na kilitumia teknolojia ya kizamani na yenye uwezo mdogo wa kuzalisha mali na hivyo kazi kubwa ilikuwa ni kusafirisha mali ghafi nje ya nchi

Alisema baada ya kufungwa kwa mitambo mipya yenye kutumia teknolojia ya kisasa kwa sasa kichakata Marbo na kutokana na mipango mizuri ya serikali, kampuni inao mpango mwingine zaidi wa kuendelea kupanua kiwanda hicho cha kipekee hapa nchini na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alisema, kuwepo kwa mradi huu sio tu kunautangaza mkoa wa Mbeya katika ramani ya Dunia bali pia taifa kwa ujumla ukizingatia bidhaa zinaendelea kuenea katika soko la ndani na la kimataifa na hivyo kutoa fursa ya kuongeza ari ya uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko.

Akieleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo baada ya kazi ya kuchakata mawe hayo makubwa aina ya Marbo na Granites, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Salim Jesa alisema, wanatengeneza tiles, meza, ngazi, na mapambo mbalimbali na kwamba kwakuwa bidhaa hizo zinatokana na mawe ya asili hakuna sababu ya kutumia kemikali (sabuni) iku kusafisha bali mtumiaji anahitaji maji tu ili kusafisha.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd Bw. Salim Jesa akitoa maelezo kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa ziara ya kimafunzo.

Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi akitazama baadhi ya bidhaa zilizotengezwa na Kiwanda hicho tayari kwa matumizi
Utengenezeji wa Marbo ukiendelea kwa uangalizi mkubwa

Afisa Utawala na Rasilimali Watu wa kiwanda hicho, Bw. Brinton Kulinga akieleleza namna bidhaa ndani ya kiwanda hicho zinavyotengeneza kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya mwisho.

Afisa Utawala na Rasilimali Watu wa kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd Bw. Brinton Kulinga akitoa taarifa ya kiwanda hicho kilichopo Iyunga Mbeya kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa ziara ya kimafunzo kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho,Salim Jessa

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd Salim Jessa akitoa maelezo kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd akionesha moja ya meza zilizotengenezwa kwa mawe ya asili kwa Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki BoT Bi. Vick Msina na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Marmo E. Granito Mines (T) Ltd akionesha moja ya bidhaa zilizotengenezwa kwa mawe ya asili kwa ajili ya mapambo ya makaburi kwa waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Benki hiyo waliotembelea kiwandani hapo kwa zaiara ya kimafunzo.

Baadhi ya waandishi wakitembelea na kushuhudia shughuli mbalimbali zinazoendela kufanyika kiwandani hapo.

Baadhi ya mawe ya asili yanayotengeneza bidhaa mbalimbali kiwandani hapo.

Baadhi ya mashine zinazotumika kutaka mawe kwa ajili ya kutngeneza bidhaa hizo.

…………………………



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...