MBUNGE wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amehoji juu ya barabara ya Kimara, Mavurunza na Kinyerezi (Kikwete Highway) iliyoahidiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete 2010, leo Februari 10, 2022.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Prof. Kitila amesema barabara hizo zilitolewa ahadi na Rais wa awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Mhandi Godfrey Kasekenya amesema ahadi zote zinazotolewa na Viongozi wakiwemo Viongozi wakuu wa nchi zimekuwa zikitekelezwa.

Amesema kuww barabara zote zilizozungumziwa na Mbunge Prof. Kitila Mkumbo zitajengwa kwa kiwango cha lami  kadiri fedha itakavyopatikana.

Amesema umuhimu wa barabara hizo umeongezeka ikiwemo ya Kinyerezi inayofahamika kama Kikwete Highway kutokana na ujenzi wa kituo cha mabasi cha Kinyerezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...