Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Ladislaus Kamoli amemtumia salaam za shukrani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kufuatia kiasi kikubwa cha pesa ambacho kimeidhinishwa kuimarisha miundombinu katika kata za Kipawa na Kinyerezi.
Mhe. Mbunge alituma salaam hizo Jumamosi 19/02/2022 alipokuwa anashuhudia makabidhiano ya Ujenzi wa barabara ya Airport Karakata (453,758,000) Kata ya Kipawa. Na Madaraja mawili muhimu ya Kinyerezi - Kifuru - Majoka (700,000,000) na Kifuru Kwa Masista (600,000,000) Kata ya Kinyerezi. Wakiwa wanajenga Madaraja kutajengwa pia barabara mbadala ya dharura yenye urefu wa 1.9km ijulikanayo Kama PUMA - MSOME kwa gharama ya Sh. 208,760,000 (Kata ya Kinyerezi)
"Tunafahamu kuwa kiasi cha pesa zaidi ya 1.5B kilichokuja kata ya Kinyerezi hakikuwa kwenye bajeti ila kutokana na Madaraja kukatika na hivyo kukatiisha mawasiliano ya wananchi wa Mtaa wa Kifuru na viunga vingine vya kata ya Kinyerezi, n.k Mhe. Rais amesikia kilio chetu na ametupatia hizi pesa ili tufungue mawasiliano na changamoto hii iishe! Tunamshukuru sana mama yetu kwa kuendelea kutusikia wana Segerea na kutupatia pesa kila tukimkimbilia" Alisema Mhe. Bonnah.
Akiongea katika makabidhiano hayo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala Eng. Silivester Chinengo aliwaeleza wananchi Namna Mhe. Mbunge alivyoshirikiana nao kuhakikisha wanaipata hiyo pesa kutoka serikalini. Alisema Madaraja tajwa hapo juu yalikatika ghafla na hivyo kupata Bilioni Moja na nusu ambayo haikuwa kwenye bajeti ili kuyajenga halikuwa Jambo jepesi. Hivyo wao Kama TARURA wanamshukuru sana Mhe. Mbunge kwa jitihada za kuhakikisha pesa hiyo inapatikana.
Kwa upande wa kata ya Kipawa, Eng. Chinengo alisema kuwa barabara ya Airport Karakata Itajengwa na TRC kupitia mradi wa SGR kuanzia Mataa ya Airport Hadi kuvuka Reli ambapo kuna Urefu wa 0.6 km na wao Kama TARURA watajenga kuanzia Relini kuelekea ndani urefu wa 0.4km
Wakiongea kwa nyakati tofauti kwa niaba ya wananchi Mhe. Aidan Kwezi (Diwani - Kipawa) na Mhe. Leah Mgitu (Diwani - Kinyerezi) wamemshukuru sana Mhe. Mbunge kwa Kazi kubwa anayoendelea kuifanya na hasa ushirikiano anaowapatia katika kutatua changamoto za wananchi katika kata zao.
Katika makabidhiano hayo walikuwepo viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutoka kata husika, Wenyeviti wa S/Mitaa na viongozi wengine wa serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...