Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Simba SC sasa imekusanyia alama nne kwenye msimamo wa Kundi D la Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya kupata sare ya bao 1-1 nchini Niger dhidi ya wenyeji US Gendermarie Nationale ya nchini humo.

Wenyeji wa mchezo huo, USGN walipata bao la kuongoza katika dakika ya 12 ya mchezo, kipindi cha kwanza kupitia kwa Mshambuliaji wake, Wilfred Gbeuli ambaye aliunganisha mpira safi baada ya mabeki wa Simba SC kufaya makosa katika eneo lao la ulinzi.

Kipindi cha pili, Simba SC walirejea kwa kufanya mashambulizi mbalimbali, huku wakifanya mabadiliko, kwa kuingia John Bocco, Bernard Morrison ambao walileta nguvu katika eneo la ushambuliaji na kupelekea kupata bao la kusawazisha dakika ya 84 kupitia kwa Morrison.

Simba SC wamepata sare hiyo ambayo sasa imewaweka nafasi ya kwanza katika msimamo, mchezo wa raundi ya tatu Simba SC itakuwa ugenini kumenyana na RS Berkane ya Morocco yenye Winga Tuisila Kisinda na Kocha Mkuu Florent Ibenge.

Hata hivyo, Simba SC imeonekana kuvutiwa na Mshambuliaji wa timu hiyo ya USGN, Victorien Adebayor ambaye ameonyesha kiwango bora katika mchezo huo, mara kwa mara akiisumbua safu ya ulinzi ya Simba SC
.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...