*Vijana wanapata ulaghai wa watumiaji wa mitandao wasiowaadilifu kwa kupatiwa taarifa za siri katika mitandao yao 

 Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imesema baadhi ya watumiaji wa mitandao wamekuwa wakiwalaghai vijana na kuwasababishia madhara mbalimbali ya katika utumiaji wa mitandao

Hayo ameyasema Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt.Jabiri Bakari ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya leseni wa Mamlaka hiyo John Daffa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni 2022 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Daffa ametoa onyo kwa wale wanaotumia mitandao vibaya na kusema sheria ziwepo huku wengine wakishitakiwa kutokana na kutumia mitandao hiyo .

Daffa amesema uwezo wa mtandao kuficha utambulisho wa mtumiaji, umewawezesha watu wenye nia ovu kujifanya kama vijana wadogo na kushawishi vijana kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo hivyo TCRA imekuwa sehemu ya wajibu wa kutoa elimu kwani matumizi ya Internet ni ushiriki jumuishi.

'"Vile vile watu hao wanaweza kuiba au kukushawishi uwatumie taarifa zako binafsi kama picha,nywila pamoja na mwaka wa kuzaliwa kuzitumia kufanya uhalifu mtandaoni ikiwa ni pamoja kufanya utapeli, kusambaza taarifa za uongo wakilenga kuchafua taswira yako au kufanya manyanyaso dhidi yako na kusababisha usumbufu kwa waathirika wa vitendo hivyo hivi,"amesema Daffa 

Amesema pamoja na mitandao ya kijamii kuwa nyenzo za kulinda usiri vijana wengi hawatumii nyenzo hiyo na hivyo kusababisha taarifa zao kuonekana kwa watu wenye nia mbaya na hivyo kuzitumia vibaya dhidi yao na kujikuta na wanaathirika kisaikolojia.

Akitoa takwimu alisema hadi Disemba mwaka Jana idadi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti imekuwa hadi 
 mawasiliano kukua.

Daffa amesema huduma za mawasiliano zitumike kwa kuhabarisha pamoja na kufungua fursa za kibiashara katika mitandao kwa kuuza bidhaa za aina mbalimbali na kusaidia nchi kuendelea kukua kiuchumi.

Amesema serikali imejipanga vyema kuandaa mazingira bora na wezeshi kwa jamii ya watanzania kushiriki ipaswavyo kwenye uchumi wa kidijitali kwa wazazi na watoto ili kuwa na mnyororo wa kutumia mitandao kwa usalama.

" Tumeshuhudia watu wengi wakiinuka kiuchumi kwa kutumia mtandao. Wengi wanaweza kufanya biashara na kuinua maisha yao wenyewe na wale waliowaajiri ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye pato la taarifa,'alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( Tehama), Connie Francis alisema Tanzania ni moja ya nchi iliyochukua hatua katika matumizi ya tehama na kuwa shirikishi.

Maadhimisho ya Siku hii ni mango wa kimataifa ulioanzishwa 2014 kwa lengo la kuhamasisha matumizi bora na salama ya mtandao wa intaneti.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Chang'ombe Demostration Husna Ramadhan amesema kupata elimu ya matumizi ya mitandao ni nzuri kwani baadhi ya vijana wanaigia kutumia vibaya kutokana na kukosa elimu hiyo.

Amesema kuwa sheria zieongezwe kuwabana watumiaji wa mitandao ili wasiweze kuharibu jamii na elimu endelee kutolewa na wanafunzi wa elimu ya msingi ili wakifika katika umri wa kumiliki simu au komputa wanakuwa na uelewa juu ya matumizi ya mitandao
Picha mbalimbali za pamoja wanafunzi wa Shule za Msingi,Sekondari na Vyuo na Meza kuu katika maadhimisho ya siku ya usalama matandao yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Washindi wa Mashindano ya Tehema wakiwa na Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya usalama mtandaon yaliyoanyika jijini Dar es Salaam.
Washindi wa mashindano ya Tehama yaliyoendeshwa na TCRA wakiwa na vyeti vyao katika maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni.
Meneja wa Huduma za Watumiaji huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akizungumza kuhusiana na huduma za mawasiliano kwa wanafunzi katika maadhimisho ya siku ya usalama mtandaoni ambayo huadhimishwa kila Desemba 8 Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Tehama wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Connie Francis akizungumza kuhusiana na TCRA inavyotoa mafunzo juu ya Tehama pamoja na kuandaa mashindano mbalimbali ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Leseni wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) John Daffa akizungumza wakati maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...