Na Amiri Kilagalila,Njombe
Serikali ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imeagiza polisi kuwakamata kama mwewe anavyokamata vifaranga na kuwashughulikia kisheria wale wote wanaosababisha ujauzito kwa wanafunzi.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani humo Mh,Andrea Tsere alipozungumza na wakazi wa kata ya Ibumi.
"Kazi ya polisi ni kukamata muarifu,muarifu anayesababisha ujauzito kwa mtoto wa shule anatakiwa kukamatwa kama mwewe anavyokamata vifaranga"Andrea Tsere
Tsere amesema waarifu hao wanatakiwa kutafutwa kokote na kukamatwa ili kukomesha vitendo hivyo.
Licha ya mkuu huyo wa wilaya kuliagiza jeshi la polisi vilevile agizo hilo amewaachia viongozi wa ngazi za vijiji na kata pamoja na kuwataka wazazi waache mara moja tabia za kusema jambo hilo liishie mtaani.
"Watoto waacheni wasome,na wale wanaume wanaozunguka zunguka huku kuaharibu watoto wakome na ninyi wazazi msifiche taarifa,hii habari ya kukubaliana,kuhongana mnasema tuyamalize nyumbani ikome"alisema Andrea Tsere
Aidha ametoa wito kwa kuvitaka vyombo hivyo vya dora alivyoviagiza kuwakamata wahalifu vitekeleze agizo hilo huku akibainisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh,Samia Suluhu Hasan anapenda watoto wote wasome.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...