Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv

 MAMLAKA ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri kuwa kutakuwa na mvua za kutosha kwa msimu wa Mvua za  Masika wa Machi hadi Mei, 2022 kwa mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Febuari 17, 2022, Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Agnes Kijazi amesema kuwa Mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi.

"Matukio ya Magonjwa ya Mlipuko na wadudu  waharibifu yanaweza kujitokeza kutokana na hali ya unyevunyevu na kutuama kwa Maji." Amesema Dkt. Kijazi

Amesema  Mvua zinatarajiwa kuanza mapema kati ya wiki ya Tatu na ya nne ya Mwezi Februari 2022 na kuisha Mwezi Mei 2022 katika maeneo mengi. 

Katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Visiwa vya Ugunja na Pemba pamoja na Visiwa vya Mafia mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya  wastani na zitaanza mapema  wiki ya tatu ya mwezi Februari, 2022 na zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya Mwezi Mei, 2022.

Dkt. Kijazi  amesema Kanda ya Ziwa Viktoria katika mikoa ya Kagera Geita, Mwanza, Shinyanga, Simuyu, Mara pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma hasa wilaya ya Kakonko na Kibondo Mvua za masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani na zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki ya tatu na ya nne mwezi Februari na kuisha nwezi Mei, 2022 katika maeneo mengi. 


Nyanda za juu Kaskazini Mashariki ambayo ni mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani na zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Februari na zinatarajiwa kuisha wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Mei, 2022.


"Huduma Mahusi za hali ya hewa kwa faida za kiuchu." Dkt. Kijazi amesema hiyo ndio kauli mbiu ya Msimu wa Mvua za Machi hadi Mei, 2022

 


Aidha Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa maeneo mengi yanayotarajiwa kuwa na Mvua za wastani na juu ya wastani kuwa na vipindi vya mvua zinazoambatana na Upepo Mkali.


Aidha TMA imetoa Ushauri kwa Sekta za Kilimo na Usalama wa chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyama pori, Usafiri na Usafirishaji, Nishati, Maji na Madini, Mamlaka za Miji, Afya, Sekta binafsi na Menejimenti za Maafa.


Licha ya hayo Dkt. Kijazi amesema kuwa joto la bahari linatarajiwa kuwa la wastani hadi chini ya Wastani katika eneo la kati la Bahari ya Pasifiki na wastani katika bahari ya Hindi.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dkt. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 17, 2022 na kutoa Utabiri wa kuwa na Mvua za Kutosha kwa Kipindi cha Mvua za Masika kwa Mikoa inayopata Mvua Mara mbili kwa Mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...