Na Rachel Mkundai, Mwanza

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata amezindua App mpya ya Hakiki Stempu ambayo inawezesha kutambua bidhaa isiyofaa kwa usalama wa afya pamoja na kuiwezesha serikali kukusanya kodi stahiki kutoka kwa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa kwa mfumo wa kubandikwa Stempu za Kodi za kieletroniki (ETS).

Akizindua App hiyo jijini Mwanza, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Kidata ametoa wito kwa watumiaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa kupakua App hiyo katika simu zao za kiganjani bure ili kuhakiki bidhaa hizo kabla ya kuzitumia kwa kulengesha simu zao kwenye stempu zilizobandikwa kwenye bidhaa husika hapo mtumiaji ataweza kupata taarifa za bidhaa hiyo imezalishwa na nani, lini, na itakuwa imepita katika mikono ya vyombo vya udhibiti wa ubora vya serikali.

Aidha, Kamishna Mkuu Bw. Kidata ameongeza kuwa hadi sasa, bidhaa zinazobandikwa Stempu za Kielektroniki za Ushuru ni pamoja na Sigara, Mvinyo wa Zabibu, Pombe Kali, Bia, Mvinyo wa matunda mengine kama vile Ndizi, Rozela, Nyanya pamoja na aina zote za vileo.

Kamisha Mkuu amefafanua kuwa bidhaa zingine ambazo tayari zinatumia mfumo huu wa stempu za kodi za kieletroniki ni vinywaji laini kama Soda, Visisimuzi (energy drinks), sharubati (juice), maji yanayowekwa kwenye chupa na bidhaa za muziki na filamu zilizofungashwa kwenye CDs/DVDs/Kanda. Jumla ya viwanda 286 tayari vimeshaunganishwa na mfumo ya stempu za kieletroniki kote nchinin na waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi ni 106.

Wakati huo huo, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Kidata amezitaja faida za mfumo wa ETS kuwa pamoja na kulinda afya ya mtumiaji kwa kujiridhisha usalama wa bidhaa kupitia app ya Hakiki Stempu, mfumo huu pia unahakikisha kodi halali ya serikali inalipwa kupitia kwa wazalishaji au waagizaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja na kuwezesha kutambuaa na kuzuia bidhaa bandia sokoni kwa manufaa ya kuwalinda wafanyabiashara wema wanaotekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria.

Vile vile Kamishna Mkuu ametoa wito kwa wazalishaji na waingizaji wa bidhaa hizo kutumia mfumo wa ETS kwa uaminifu kwani mfumo huu una faida nyingi kwao ikiwemo kulinda bidhaa zao sokoni dhidi ya bidhaa bandia pamoja na kusaidia makadirio ya kodi kwa haki.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...