Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

UMOJA wa Vijana wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam wameanda Semina Maalum ambapo pamoja na mambo mengine wanatarajia kutumia semina hiyo kuliombea Taifa pamoja na kuabudu.

Mwenyekiti wa Umoja huo Dayosisi ya Dar es Salaam John Kibata ametoa taarifa ya semina hiyo na kueleza kwamba semina hiyo itaongozwa na Baba Askofu wa Dayoyosi ya Dar es Salaam Sosthenes Jackson Sosthenes.

Amefafanua Semina hiyo  inatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Februari 5 mwaka huu kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa Saba mchana katika Mtaa wa Mt.Batolomayo wilayani Ubungo.

Kibata amesema "Wapendwa sana katika Kristo Yesu,  Vijana wote  ( Pamoja na Viongozi wote TAYO) ndani ya Dayosisi yetu ya Dar es salaam ni matumaini yangu kuwa tunaendelea vyema na majukumu ya kila siku na huduma ya Mungu kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

"Nawataarifu rasmi na kuwaalika katika tukio maalum la Semina ya Vijana wote Dayosisi ya Dar es salaam litakalofanyika siku ya Jumamosi hii tarehe 05/02/2022 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa Saba mchana katika Parishi/ Mtaa wa Mt.Batolomayo Ubungo."

Ameongeza katika semina hiyo kutaambatana na matukio mbalimbali yakiwemo ya Kusifu na kuabudu, Uimbaji wa kwaya ,Maombi maalum ya makundi mbalimbali ya Vijana sambamba na maombi maalum kwa Kanisa na Taifa letu.

Kutokana na umaalum wa semina hiyo Kibata amewaomba Vijana wenzake kuungana kwa pamoja sambamba na kuwasihi kuendelea kuwaalika na wengine.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...