Na Mwandishi Wetu,Lindi

WADAU mbalimbali ambao  wanaoshiriki Mafunzo ya watoa huduma katika Mnyororo wa Utalii kupitia Mradi wa UVIKO 19 awamu ya kwanza yanayoendelea Wilayani Rangwa mkoani Lindi wameiomba Serikali kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii kuweka utaratibu wa kuwapelekea mafunzo hayo mara kwa mara ili kuendelea kuwajengea uwezo katika maeneo mbali mbali katika Sekta hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo hayo baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuchukua hatua katika kukabiliana na janga UVIKO 19 na kwamba uwepo wa mafunzo hayo kutawajengea uwezo wa kufahamu namna ya kukabiliana na janga hilo.

Kwa upande wake Hamisi Slim Othman ambaye ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo, ameeleza kuwa janga la UVIKO 19 limekuwa tishio hasa katika sekta ya Utalii na kwamba ujio wa mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa kutokana na uwepo wa wageni wanaoingia nchini na kupata huduma katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Amesema wao kwa niaba ya Serikali ya Wilaya ya Ruangwa wamefarijika sana kiasi ambacho hatuna cha kuilipa Serikali."Tumeona kumbe kuna muingiliano baina ya kuona huduma zetu na hili wimbi la UVIKO - 19 lakini tunakishukuru Chuo cha Taifa cha Utalii kutuletea Mafunzo haya tumenufaika sana kwa kufahamu namna gani ya kuwahudumia wageni wanaofika katika maeneo yetu ya kazi" amesema Othman.

Wakati Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo mjasiriamali Lesa Rogers, amesema kuwa amenufaika sana na mafunzo hayo na kwamba elimu hiyo ataitumia kwa kuwaelimisha watu wengine waliokosa fursa hiyo na kwamba amefarijika sana kupata chanjo ambayo inatolewa kwa hiyari katika mafunzo hayo.  

"Chuo cha Taifa Cha utalii tunakishukuru kutuletea mafunzo haya mimi kama Mjasiriamali nimenufaika sana kwa kufahamu vitu vingi kuhusu UVIKO 19 hata sasa naweza kuwafundisha na wenzangu namna ya kujikinga na Ugonjwa huu," amesema Lesa Rogers.

Aidha Mkuu wa Idara ya Ukarimu na Mkufunzi Mwandamizi katika Sekta ya huduma kwa wateja na Mapokezi Jesca Willium amesema kuwa mafunzo hayo yanayoendelea Wilayani Ruangwa yamelenga katika kuwajengea uwezo washiri hao kufahamu mbinu mbalimbali wanazoweza kuzitumia katika kipindi hiki cha UVIKO -19 na kutambua namna ya kutoa huduma zao na kushughulikia changamoto za wateja kwa ujumla.

"Leo tumeendelea na Mafunzo ambapo washiriki wameweza kujengewa uwezo wa mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya usafi sehemu zao za kazi na wao wenyewe kama watoa huduma kwa kutambua kuwa ni jinsi gani usafi unavyoweza kuwa suluhisho katika kipindi hiki cha UVIKO 19 na usalama wa chakula kwa ujumla" amesema Jesca.

Mafunzo hayo ya siku tano yanayoratibiwa na Chuo cha Taifa cha Utalii yanawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa lindi na kuendelea katika mikoa nane ya Tanzania Bara.




Mkuu wa Idara ya Ukarimu na Mkufunzi Mwandamizi katika Sekta ya huduma kwa wateja na Mapokezi Jesca Willium akiendelea na mafunzo kwa wadau wa mnyororo katika sekta ya Utalii wilayani Ruangwa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...