BALOZI wa India Tanzania, Binaya Pradhan ametoa neema kwa watanzania na ushirikiano katika sekta za Kilimo, Bandari, Gesi na Mafuta, Viwanda Vidogo, hospitali na Elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 25 amesema kuwa katika sekta ya kilimo mazao ambayo hayatozwi kodi ni pamoja na Parachichi, Korosho, Mbaazi kunde na dengu.
Amesema kuwa watanzania wachukue hiyo kama fursa kwaajili ya kuuza mazao hayo India na kukuza ushirikiano wa kiuchumi.
Kwa upande wa Maji Balozi Pradhani amesema kuwa ushirikiano ulishaanza tangu mwaka 2019 ambapo wataalamu kutoka India walianza kutoa mafunzo ya utunzaji wa maji na kuwapa mbinu bora za usambazaji huduma hiyo.
Kwa uwekezaji wa Bahari amesema kuwa wataimarisha ulinzi na usalama katika bahari kwasababu Tanzania na India zote zinatumia bahari ya hindi na kushirikiana katika kuitunza.
Amesema ushirikiano huo utagusa katika sekta ya Uvuvi viwanda vya ufungaji na uchakataji samaki pamoja na sekta ya Utalii na vitega uchumi vyote vilivyopo baharini.
Katika sekta ya Elimu na hospitali amesema ushirikiano huo upo kwasababu wameshajenga Viwanda cha dawa nchini na wanashirikiana na hospitali ya Bugando Mwanza na upande wa Elimu India inatoa ufadhili wa watanzania kwenda kusoma India.
Balozi Pradhan amesema kwenye eneo la bandari kampuni kubwa za India za usafirishaji na kuhudumia shehena zitawekeza wakati kwenye elimu wanaangalia fursa za kufungua taasisi zaidi za elimu na majadiliano na serikali yanaendelea kufanikisha uwekezaji zaidi.
Amesema India ni mwekezaji mkubwa nchini na kwamba taifa hilo sasa litaongeza uwekezaji kwenye maeneo mapya ya kimkakati, akitaja bahari, uwekezaji kwenye bandari, umeme, gesi na mafuta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...