Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Wauguzi wa Zahanati ya Mihambwe iliyopo Kata ya Mihambwe Tarafa ya Mihambwe wamepongezwa kwa kuongoza wa kwanza kiwilaya kwa wingi wa utoaji wa huduma ya chanjo ya Uviko 19 kwa Watu.

Hayo yamebainishwa Leo Jumanne Februari 1, 2022 wakati wa ziara iliyofanywa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kwenye Zahanati ya Mihambwe ambaye alienda kuwapongeza Wauguzi na kusikiliza changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzipatia utatuzi.

"Kwanza Serikali tunawapongeza kwa utoaji wa huduma bora nyakati zote. Pili sio kwa umuhimu, Serikali tunawapongeza kwa uongozaji kiwilaya uchanjaji chanjo ya Uviko 19 (Corona 19) ambapo Zahanati ya Mihambwe mmekuwa wa kwanza kiwilaya, mmechanja jumla ya Watu 1405 na anayefuata amechanja Watu 342. Hongereni sana, nawasihi muendelee kuwa bora zaidi."

"Pia nawapongeza Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe kwa kuitikia na kuunga mkono kivitendo wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kuchanja chanjo ya Uviko 19 kwa hiyari yao." Alisema Gavana Shilatu.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Dk. Merkezedek Liyama alishukuru kwa kuona mchango wa utendaji kazi wao umeonekana na kuthaminiwa.

"Sisi tunashukuru kwa kuyaona yale tunayoyafanya na tunahaidi kuendelea kupambana kutoa huduma bora pasipo kuchoka." Alisema Dk. Liyama

Tarafa ya Mihambwe ina Zahanati 5 na Kituo cha Afya kimoja ambacho kipo hatua ya ukamilishwaji kujengwa tayari kuanza huduma.

Katika ziara hiyo ya kutembelea Zahanati ya Mihambwe, Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata Mihambwe na kuhaidi kutatua changamoto zinazowakabili.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...