Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Kassim
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya mbio za
Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2022.
Taarifa
iliyotolewa na waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon ilisema Waziri
Mkuu ataongoza maelfu ya washiriki na watazamaji katika maadhimisho
hayo ya miaka 20 Mjini Moshi Jumapili Februari 27, 2022.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, Waziri Mkuu anatarajiwa kuongozana na Waziri wa
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na
viongozi wengine wa kitaifa na mkoa.
“Maandalizi
yote yamefikia hatua nzuri huku tukisubiri kumpokea Waziri Mkuu katika
maadhimisho haya ya miaka 20,” walisema waandaaji hao.
Kwa
mujibu ya waandaaji hao, Mh. Majaliwa anatarajiwa kushiriki katika mbio
za Grand Malt 5Km kabla ya kuendelea na shughuli za sherehe ya miaka 20
katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU).
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi, ambaye bia yake
ni mdhamini mkuu wa Kilimanjaro marathon, alisema wanayo furaha kuungana
na Waziri Mkuu katika maadhimisho ya miaka 20 kwani inaonesha uzito wa
shughuli hii.
“Hii
inaonesha ni jinsi gani Kilimanjaro Marathon imekuwa mwaka hadi mwaka
na hata kuwavutia viongozi wa kitaifa,” alisema huku akitoa wito kwa
washiriki kuendelea kujifua vizuri na kuhudhuria kwa wingi.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water.
Wasambazaji
rasmi ni GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC
Automobiles na Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na
kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions
Limited.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...