Na Amiri Kilagalila,Njombe
Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Njombe kimeagiza kujengwa ofisi za Chama hicho ngazi ya kata katika maeneo yote ya wilaya hiyo ili kuendelea kutofautisha ukubwa wa Chama hicho na vyama vingine vya siasa.
Agizo hilo limetolewa na katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Njombe bwana Sure Mwasanguti kwa viongozi wa Chama hicho mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa ofisi za Chama kata Maguvani halmashauri ya mji wa Makambako.
“Chama chetu kipindi hiki tunahitaji kuwa na ofisi maeneo yote,hatuhitaji Chama kikongwe kama hiki kinajibanza kwenye viofisi na kufanana na vyama vingine ambayo vina miaka kumi ambao tuna vifundisha”alisema Mwasanguti
Licha ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo Chama cha Mapinduzi kimewapokea wanachama takribani 100 kutoka jimbo la Makambako waliokuwa vyama vya upinzani akiwemo mwenyekiti chama cha madereva wa bajaji Bwn.Bonifasi Sanga aliyekuwa akitajwa kufanya hujuma kubwa wakati uchaguzi.
“Ukisikiliza hotuba ya ndugu yetu ambaye amerejea unaona kabisa kazi kubwa iliyofanyika na haya aliyosema sio mengi,mkikaa naye ofisini atawaambia na amezungumza moja la kuzulumu mikutano tunamshukurua sana ndugu yetu na tunakukaribisha Chama cha Mapinduzi”aliongeza Mwasanguti
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wapya waliojiunga na Chama cha Mapinduzi bwana Sanga amesema wameamua kwa ridhaa yao kujiunga na Chama hicho na kuomba radhi kwa makosa yote waliowahi kuyafanya awali.
“Mimi nimeshawahi amrisha vijana wetu kwenda kuvunja halmashauri tulikwenda pale na kuvunja vioo,kwa kuwa nilikuwa CHADEMA kwa hiyo nilikuwa na roho ya ushetani leo nakiri naomba mnisamehe sana”alisema Bonifasi Sanga
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa ambaye ni diwani wa kata ya Maguvani amesema utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho unaendelea vizuri ndio maana wanaendeleaa kupata wanachama wapya.
“Makambako ni sehemu sahihi sana kwa Chama cha Mapinduzi ndio maana wenzetu wanaamua kurudi,wametafakari na kuona tunachokifanya kinaonekana kwa hiyo hakuna sababu ya kuendelea kupinga,tuwakaribishe sana hawa ndugu zetu kwa kuwa sisi hatuna ubaguzi”alisema Mfikwa
Kutokana na wimbi hilo la wanachama kurejea,mwenyekiti wa Chama cha madereva bajaji ameahidi kushawishi vijana zaidi ya 900 waliopo kwenye chama chama chao wasio kuwa wanaccm kujiunga na Chama cha Mpainduzi.
Katibu wa CCM wilaya ya Njombe bwana Sure Mwasanguti akionyesha moja ya kadi ya Chama ya mwanachama wa CHADEMA aliyehamia chama cha Mapinduzi
Katibu wa CCM wilaya ya Njombe bwana Sure Mwasanguti akisogea kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa ofisi za Chama hicho kata ya Mguvani.Katibu wa CCM wilaya ya Njombe bwana Sure Mwasanguti akifungua jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi za chama hicho kata ya Maguvani mjini Makambako.Kushoto ni bwana Bonifasi Sanga akikabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi baada ya kupokewa na viongozi wa Chama hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...