Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevionya vyombo vine vya habari pamoja na kuvitoza faini y ash milioni mbili kutokana na mtangazaji kuvuta sigara wakati wa kipindi, kutangaza maudhui ya matumizi ya dawa zitokanazo na waganga wa kienyeji na ushirikina,
Pia kutangaza maudhui yasiyo na staha kwa kujadili masuala yenye viashiria vya uanyaji wa ngono na yasiyofaa hasa kwa watoto na wasikilizaji pamoja na kurusha maudhui yasiyo na staha yenye viashiria vya ufanyaji wa ngono.
Akisoma uamuzi wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Maudhui Habbi Gunze alisema Kituo cha Dizzim Televisheni kinatuhumiwa kukiuka sheria ya mamlaka hiyo juu ya ushindani wenye tija ambapo mtangazaji wa kipindi alisoma kwa undani habari kutoka katika gazeati moja nchini.
Alisema kitendo cha kuacha kusoma vichwa vya habari na kujikita katika kusoma maudhui ya magazeti kwa undani kunaondoa ushindani wa kibiashara katika tasni aya habari.
Alisema kutokana na ukiukwaji huo, imetoa onyo kwa televishioni hiyo ya Dizzim pamoja na kuamuru kulipa faini ya shilinga laki tano ndani ya siku 21 tangu kutolewa kwa uamuzi huo.
Pia alisema Times FM Redio ambapo Februari 3 mwaka huu ilirusha kipindi cha ‘Pillow talk’ ambacho kilikuwa na maudhui kuhusu utabiri wa nyota kinyume na kanuni za utangazaji.
“Mnamo Februari 3 mwaka huu, Times Radio FM kupitia kipindi cha CCTV Camera walirusha maudhui ya uongo kuhusu matumizi ya dawa zitokanazo na waganga wa kienyeji na ushirikina kinyume na kanuni za utangazaji,” alisema.
Alisema baada ya kutafakari kwa kina maelezo yaliyowasilishwa na Times Fm Radio kamati ya maudhui imeridhika pasi na shaka kuwa kituo hicho kimekiuka kanuni za utangazaji wa maudhui ya redio na televisheni hivyo imetoa adhabu ya onyo kali.
Akitoa uamuzi wa Entertainment FM Radio alisema kuwa kituo hicho kinatuhumiwa kutangaza maudhui yasiyo ya staha kwa kujadili masuala yenye viashiria vya ufanyaji wa ngono na yasiyofaa hasa kwa watoto na ambayo hayakupaswa kutangazwa katika muda ambao watoto wanaweza kuwa sehemu ya wasikilizaji.
Alisema baada ya kuwasikiliza kamati imebaini walikiuka kanuni za mawasiliano ya kieletroniki na posta, hivyo iliwapa onyo na kulipa faini y ash. Milioni moja ndani ya siku 21.
Alisema shauri lingine ni dhidi ya Dina Marios Baby Coconut Oil online TV, kuwa alirusha maudhui yasiyo na staha na yenye viashiria vya ufanyaji wa ngono.
Alisema baada ya kumsikiliza kamati ilimpa onyo na kumwamuru kulipa faini y ash laki tano ndani ya siku 21.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habby Gunze akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana vyombo vya habari vilivyokiuka maudhui ya Utangazaji ,jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...