Kampuni Pendwa nchini ya Huduma za mawasiliano ya Halotel Tanzania kupitia mfumo wake wa Huduma za kifedha wa HaloPesa inaendelea kuwahamasisha wateja wake na watu wote nchini kwa ujumla kuendelea kutumia huduma za kifedha kwa njia ya simu hasa huduma za HaloPesa kwa kuzindua rasmi leo promosheni inayojulikana kwa jina la SHINDA NA HALOPESA. Promisheni hii inawapa wateja wa HaloPesa fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu pamoja na Pikipiki maarufu kama BodaBoda.

Ikiwa ni huduma inayokuwa kwa haraka zaidi ,HaloPesa imesambaa na kuenea kote nchini na imeendelea kutoa huduma zake bora na zenye ubunifu, rahisi kutumia na zaidi sana kwa gharama nafuu kwa wateja wake wote waliopo mijini na vijijini kote nchini.

Akiongea katika uzinduzi wa Promisheni hii, Naibu Mkurugenzi mkuu wa HaloPesa, Mr. Magesa Wandwi alisema “ tunafurahi wakati wote kuwa katika Tasnia hii ya utoaji wa Huduma za Kifedha kidigitali, huduma ambazo zinawapa wateja wetu na umma wa watanzania kwa ujumla fursa ya kufanya miamala kwa njia ya simu ikiwa ni pamoja na kutuma Pesa kutoka HaloPesa kwenda HaloPesa, HaloPesa kwenda mitandao mingine , HaloPesa kwenda Benki, Kununua muda w maongezi na vifurushi,Kulipia bili na Malipo mbalimbali, kulipia huduma za serikali, Kutoa Fedha kwa mawakala wetu na katika ATM n.k. Zaidi ya wateja wetu milioni 3.5 wameendelea kufurahia huduma zetu kote nhini wakati wote.

Tumekuja na Promosheni hii ya SHINDA na HALOPESA ili kuendelea kutia chachu na hamasa kwa wateja wetu na umma wa watanzania wote kuendelea kutumia huduma za kifedha hasa HaloPesa ikiwa ni katika malengo yaleyale na nia yetu thabiti na ajenda ya serikali kwa ujumla kuwafanya watanzania wengi zaidi kutumia mifumo rasmi ya kifedha .. Aliongeza Magesa.

Promeshini hii itakayoendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa, Jumla ya wateja 72 watajishindia zawadi , wateja 64 watajishindia zawadi za fedha Taslimu zitakazo tolewa kila siku kwa kipindi chote cha wiki 8, wapo watakao jishindia Tsh 50,000 na wengine Tsh.100,000 kwa kila siku. Wateja 8 watajishindia Pikipiki (BodaBoda) mpya kabisa. kila mmoja pikipiki moja kila wiki kwa kipindi chote cha wiki 8.

Tunawakaribisha na kuwahimiza wateja wetu wote na wale ambao hawajaanza kutumia Huduma ya HaloPesa kuchangamkia promosheni hii kwa kufanya miamala mingi wawezavyo ya HaloPesa ikiwa ni pamoja na kutuma Pesa kutoka HaloPesa kwenda HaloPesa, HaloPesa kwenda mitandao mingine , HaloPesa kwenda Benki, Kulipia bili na Malipo mbalimbali, kulipia huduma za serikali, Kutoa Fedha kwa mawakala wetu na katika ATM,HalaYako ,kununua muda wa maongezi na vifurushi ili kijiongezea fursa na nafasi zaidi ya kuibuka washindi na kujipatia zawadi za hizi za fedha Taslimu na BodaBoda. Alisema Magesa.

HaloPesa ni chaguo la wateja ,tunafurahi wakati wote kuwapatia huduma bora,rahisi na zenye gharama nafuu, “HaloPesa ni familia, HaloPesa ni Maisha, Ishi nayo”.



 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa HaloPesa, Mr. Magesa Wandwi na Roxana Kadio Afisa Masoko Halopesa wakizindua rasmi kwa kukata utepe leo katika makao makuu ya ofisi ya Halotel ikiwa ni ishara wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya ya Halopesa inayojulikana kwa jina la “Shinda na Halopesa” inayowapa wateja wote wa Halopesa walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Pikipiki maarufu kama BodaBoda kila wiki. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa.



Naibu Mkurugenzi Mkuu wa HaloPesa, Mr. Magesa Wandwi, akiongea na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya ofisi ya Halotel wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya ya Halopesa inayojulikana kwa jina la “Shinda na Halopesa” inayowapa wateja wote wa Halopesa walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Pikipiki maarufu kama BodaBoda kila wiki. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa. Kulia ni Roxana Kadio Afisa Masoko Halopesa na kushoto ni Joseph Jackson Mkuu wa kitengo cha Biashara Halopesa.

Afisa Masoko wa HaloPesa, Ms. Roxana Kadio, akiongea na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya ofisi ya Halotel wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya ya Halopesa inayojulikana kwa jina la “Shinda na Halopesa” inayowapa wateja wote wa Halopesa walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Pikipiki maarufu kama BodaBoda kila wiki. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa HaloPesa, Mr. Magesa Wandwi na kushoto ni Joseph Jackson Mkuu wa kitengo cha Biashara Halopesa.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa HaloPesa, Mr. Magesa Wandwi  (wa pili kulia) na Roxana Kadio ( Kulia kwenye pikipiki) Afisa Masoko Halopesa, Joseph Jackson ( kushoto kwenye pikipiki) Mkuu wa kitengo cha Biashara Halopesa wakiwa kaika picha ya pamoja leo, katika makao makuu ya ofisi ya Halotel ikiwa ni ishara wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya ya Halopesa inayojulikana kwa jina la “Shinda na Halopesa” inayowapa wateja wote wa Halopesa walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Pikipiki maarufu kama BodaBoda kila wiki. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa.

 Afisa Masoko wa HaloPesa, Ms. Roxana Kadio (kulia kwenye pikipiki), Afisa Halopesa Ms. Happy Mzena wakiwa katika picha ya pamoja juu ya pikipiki ambazo nui mfano wa zitakazotolewa wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya ya Halopesa inayojulikana kwa jina la “Shinda na Halopesa” inayowapa wateja wote wa Halopesa walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Pikipiki maarufu kama BodaBoda kila wiki. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...